Rais wa Uturuki Erdogan alisisitiza kanuni za kidemokrasia na utashi wa taifa katika hotuba ya baada ya uchaguzi. / Chanzo cha picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisisitiza umuhimu wa demokrasia na utashi wa taifa, bila kujali matokeo ya uchaguzi.

Akizungumza na wafuasi wake mjini Ankara mapema siku ya Jumatatu muda mfupi baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, Erdogan alisema kuwa taifa la Uturuki limetumia sanduku la kura kuwasilisha ujumbe wake kwa wanasiasa.

"Bila kujali matokeo, mshindi wa uchaguzi huu ni demokrasia yetu na utashi wa kitaifa," Erdogan alisema.

Pia alitoa shukrani zake kwa wale waliounga mkono chama na muungano wake, pamoja na wananchi wote waliotumia haki zao za kidemokrasia.

Akisisitiza kanuni za kidemokrasia, Erdogan alisisitiza utiifu wake kwa matakwa ya taifa na kubainisha kuwa chama chake kimekuwa katika upande wa demokrasia na sanduku la kura.

"Leo hii, tunatenda kwa hisia sawa za uwajibikaji na hatutambui mamlaka yoyote juu ya matakwa ya taifa," Erdogan alisema.

'Kujikosoa'

Baada ya Baraza Kuu la Uchaguzi kutangaza sehem ya matokeo, Rais Erdogan alisema kuwa chama chake kitakubali matokeo ya uchaguzi.

“Hatutadharau uamuzi wa taifa letu na kuchukua hatua kinyume na matakwa ya taifa,” alisema.

Rais Erdogan alikiri kwamba chama chake hakingeweza kufikia "matokeo tuliyotaka na tuliyotarajia kutokana na mtihani wa uchaguzi wa eneo hilo."

“Tutatathmini matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa uwazi katika chama chetu na tutajihusisha na kujikosoa.

Zaidi ya hayo, Rais Erdogan alisisitiza umuhimu wa kujenga upya uaminifu na kuunda uhusiano wenye nguvu na watu.

Upinzani wanyakua ushinda miji muhimu

Chama kikuu cha upinzani cha Türkiye kiliendelea kudhibiti miji muhimu na kupata mafanikio kwingineko katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Huku zaidi ya asilimia 90 ya masanduku ya kura yamehesabiwa, Meya wa Istanbul Ekrem Imamoglu wa CHP, alikuwa akiongoza kwa kura nyingi katika mji mkubwa na kitovu cha uchumi cha Uturuki, kulingana na Shirika la Anadolu.

Mansur Yavas, meya wa mji mkuu, Ankara, alihifadhi kiti chake kwa miaka mingine mitano, matokeo yalionyesha.

Kwa jumla, CHP ilishinda manispaa ya majimbo 36 kati ya 81 ya Uturuki, kulingana na Anadolu.

TRT World