Altun alisisitiza kuwa vitengo vya serikali, vinavyoratibiwa na Kurugenzi ya Mawasiliano, vinafanya kazi kupambana na taarifa potofu na kuenea kwa madai ya uwongo na ghiliba kwenye mitandao ya kijamii. /Picha: AA  

Mkuu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, Fahrettin Altun, ameonya dhidi ya uchochezi zinazolenga kuongeza hali ya mvutano kati ya wakimbizi wa Syria walioko Uturuki.

"Uchochezi huo umeongeza hali ya sintofahamu kuhusu wakimbizi wa Syria na inafuatilia kwa karibu," alisema Altun katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X, siku Jumatatu.

Aliongeza kuwa, makundi kadhaa, yakiongozwa na yale yenye chuki dhidi ya Uturuki, yanajaribu kuvuruga amani kupitia uchochezi wao.

"Baadhi ya makundi, yenye kuongozwa na wale wenye chuki na Uturuki, wanajaribu kuvuruga amani ya nchi yetu kwa kutumia uchochezi wenye kupima utulivu wetu. Malengo yao hayatotumia, kutokana na juhudi za vitengo vyetu," alibainisha Altun.

Altun alisisitiza kuwa, vitengo hivyo, vikiongozwa na Kurugenzi ya Mawasiliano, vinafanya kazi kupambana na taarifa za uongo na ulaghai kwenye mitandao ya kijamii.

Akiwaasa wananchi kuwa makini na taarifa hizo za uzushi, alisema , "Tunawaasa wananchi wetu waache kuamini vyanzo vya taarifa hizo na badala yake kuamini na kutegemea vyanzo rasmi, hususani vile vinavyotokana na mamlaka zetu."

TRT Afrika