Hii ni mara ya kwanza pambano la kushindaniwa la ndoni linaandaliwa kisiwani humu tangu marufuku iliyowekwa miaka sitini iliyopita / Picha:  Reuters 

Haji Nasibu anayo tiketi yake mfukoni ameninunua tangu siku tatu zilizopita.

Ananiambia kama sio shabiki namba moja, basi ni miongoni mwa mashabiki wakubwa zaidi wa ndondi kisiwani Zanzibar.

''Yaani mimi na vijana wenzangu hap amtaani tangu juzi tumeshika tikiti zetu,'' anasema. ''Najiandaa tu kidogo hapa natoka niwahi mapema stadium nisije kuchelewa.

Haji ni miongoni mwa maelfu ya mashabiki wengine watakao safiri kutoka sehemu mbali mbali ndnai ya Zanzibar, Tanzania bara na hata baadhi kutoka nje ya Tanzania kwa ajili ya mapambano makali ya ndondi yatakayofanyika Jumapili hii katika uwanja wa Mao Tse Tung, Michenzani.

''Class....Ibrahim Class ndiye wangu...'' anadakia kujibu hata kabla sijamaliza kumuuliza. ''Mim inamjua sana Class. Nimemfuatilia sana pambano lake, najua ngumi zake, maana ana nidhamu na utulivu. Anayo tknik kali sana kwa hiyo najua atashinda.'' Anaongeza Haji.

Mapambano 8 yamenadaliwa katika uwanja wa Mao Tse Tung Michenzani Zanzibar / Picha : X - Ibrahim Class 

Ibrahim Class ameorodheshwa kupambana na Hamis Muay Thai, Mzanzibari mwenzake.

Marufuku ya miaka 60

Vijana wa Kisiwani Zanzibar wamejawa na hamu wakitajia matumbuizo ya kipekee.

Hii ni mara ya kwanza pambano la kushindaniwa la ndoni linaandaliwa kisiwani humu tangu marufuku iliyowekwa miaka sitini iliyopita na uatawala wa Rais wa kwanza Abedi Amani Karume.

Rais Karume aliuchukia mchezo huu na kuutaja kuwa wa kikatili na hauendani na maadili ya kimila kisiwani humo.

Utawala uliopo sasa unalenga kukuza uwekezaji hasa wa kigeni kupitia sera ya uchumi wa bluu, ambao unalenga Utalii na michezo. Miongoni mwa juhudi zilizofanywa na Rais Hussein Mwinyi ni kufufua na kukuza michezo mbali mbali ikiwemo ndondi.

Lakini msisimko pia umejaa Unguja kufuatia habari kuwa Mndonga naye anajitosa ugani akibadilishana ngumi na Muller Jr.

Kama kawaida yake Mandonga ana uvuto anaposhiriki pigano lolote na amekuwa akijiandaa kisiwani humo.

Hii ni baada ya kupewa idhini na shirikisho la ndondi tanzania waliomfanyia uchunguzi w akiafya na kusema yuko sawa kupigana tena.

Awali kulikuwa n atetesi juu ya hali ya afy aya akili ya Mandonga baada ya kulazwa kwa KO mara mbili mfululizo ndani ya mwezi mmoja.

Haji anapojiandaa kwa pambano la usiku wa leo Jumapili, anakumbuka utamu wa kujionea mwenyewe pigano kama hili.

''Mara ya mwisho nilisafiri hadi Daresalaam miezi mitatu iliyopita, nikifuata pigano la Mzanzibari Kassimu aliyekwenda kukutana na Mghana huko. Tulimpiga chini Mghana huyo. Ilikua raha ajabu.'' Anasema Haji.

Wengine watakao pambana ni Mzanzibari Dula Mbabe ambaye anamenyana na Banja.

Kuletwa kwa pigano kama hili kisiwani Zanzibar kunawapa vijana wengi motisha kuendeleza mchezo wa ndondi. Ila kwa leo macho yote ni uwanjani kila mmoja akimshabikia mwana ndondi wake.

TRT Afrika