Mandonga ansifika kwa mashamsham yake kabla ya pigano ambapo ana uzoefu wa kulipatia ngumi lake jina Picha: Ultrafight 

Bondia maarufu wa Tanzania Karim Mandonga hatimaye amepata pigo lake la kwanza nchini Kenya baada ya Mkenya Daniel Wanyonyi al maarufu 'mwana wefwe' kumpa dozi za 'ngumi dusra' yaani 'ngumi nzito' katika pigano lao la marudio lililofanyika mjini Nairobi.

Pambano kati ya Wanyonyi na Mandonga la ndondi la ubingwa la uzani wa kati halikuwa na taji, japo limewavutia mashabiki kupita kiasi kutoka Afrika Mashariki Picha : Ultra fight series  

Wanyonyi, alifanikiwa kulipiza kisasi dhidi ya Mandonga kwa kumtwanga katika pambano lao la marudio baada ya kupoteza mchezo wao wa awali mwezi Januari mwaka huu.

"Anataka anapigwa, hataki, anapigwa. Raundi hii atakuwa anaongea akiwa chini, sipigi moja, napiga mbili."

Mandonga

Bingwa huyo wa zamani wa Shirikisho la Ngumi barani Afrika (ABU), Wanyonyi, alifanikiwa kumshinda Mandonga kwa wingi wa alama katika pigano la wawili hao lililoandaliwa na 'Ultrafight series promotions,' katika jengo la Sarit, jijini Nairobi.

Kwa kweli ninafurahi sana, na ninawashukuru mashabiki na waandalizi wa pigano, kwa kuwa na imani na mimi baada ya kupoteza pigano la kwanza. Nimedhihirisha siku hiyo hali yangu haikuwa sawa. Huu ushindi una maana kubwa sana kwangu na sasa lengo langu ni kurudisha mkanda wangu.

Wanyonyi

Waziri wa Michezo nchini Kenya Ababu Namwamba, alikuwa miongoni mwa mashabiki waliompongeza Wanyonyi kufuatia ushindi wake wa kulipiza kisasi dhidi ya mandonga.

Ingawa pambano hilo lao la ndondi la ubingwa la uzani wa kati halikuwa na taji, lilishuhudia mchuano wenye mvuto

"Daniel Wanyonyi amepokea ushindi kwa uamuzi wa pointi, lakini mimi nina uhakika kabisa kwamba Wanyonyi sio mtu wa kufuruguta kwangu, mimi Mandonga mtu kazi, ni mtu wa kazi. Niko tayari kwa mechi ya 3 na nakuja kutangaza ubingwa ndani ya papa hapa Nairobi. Hata ikiwekwa rematch, nitapiga knock out tu.

Mandonga

Mashabiki wa Ndondi wanasubiri kwa hamu kuona iwapo Wanyonyi na Mandonga wataingia ulingoni kupigania taji rasmi la shirikisho la ndondi Afrika.

TRT Afrika