Wanariadha wa Kenya na Ethiopia wapokewa nyumbani kwa shangwe

Wanariadha wa Kenya na Ethiopia wapokewa nyumbani kwa shangwe

Wanariadha wa Kenya na Ethiopia wapokewa nyumbani kwa shangwe
Mashindano ya Riadha ya Dunia 2023: Mkenya Mary Moraa mshindi wa dhahabu mbio za mita 800 kwa wanawake / Picha: AFP

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa wa Bolem, wanariadha wa Ethiopia walipata makaribisho ya shujaa baada ya kuwasili mapema leo asubuhi.

Timu hiyo iliyosajili matokeo ya kuvutia katika Mashindano ya 19 ya Riadha ya Dunia, ilikaribishwa na viongozi wakuu wa serikali ya Ethiopia akiwemo Waziri wa Utamaduni na Michezo, Kejela Merdasa, Waziri wa mambo ya nje Balozi Birtukan Ayano, Waziri wa masuala ya wanawake na jamii, Ergoge Tesfaye na wanachama wa jumuiya ya riadha.

Jijini Nairobi, timu ya Kenya ilirudi baada ya kunyanyua medali 10 (tatu za dhahabu, tatu za fedha na nne za shaba) ikiongozwa na bingwa wa dunia Faith Kipyegon wakiwasili katika uwanja wa JKIA kutoka Budapest, Hungary.

TRT Afrika