Kiplagat mwenye umri wa miaka 23, alijiongezea dhahabu ya dunia ya mbio za marathon katika taji la Michezo ya Jumuiya ya Madola alilotwaa mwaka jana mjini Birmingham / Picha X - World Athletics 

Victor Kiplagat alipepea akikata upepo na joto lililopiga mji wa Budhapest, ambapo inaaminiwa leo kuwa siku yenye joto zaidi katika mji huo, na kutwaa ushindi kwa saa 2:08:53

Huu ni ushindi wa pili kwa Uganda ambapo miak akumi iliyopita Mganda mwenzake Stephen Kiprotich alinyakua taji mjini Moscow mwaka 2013.

Kiplagat mwenye umri wa miaka 23, alijiongezea dhahabu ya dunia ya mbio za marathon katika taji la Michezo ya Jumuiya ya Madola alilotwaa mwaka jana mjini Birmingham

Shindano hilo linasemekana kuwa gumu mwaka huu, kutokana na hali ya joto ambapo waandaaji walilazimika kupunguza muda wa mbio za watu wa kawaida kutoka kilomita kumi hadi sita kuwakinga na dhorubu hilo.

Kiplagat alionekana kujawa na raha alipovuka ukamba wa mwisho na kunyakua bendera ya Uganda kutoka kwa maafisa wa timu yake na kuipeperusha hadi mwisho, akishangilia ushindi wake mkubwa zaidi katika maisha yake.

"Ilikuwa siku yangu leo, kulikuwa na joto lakini hali ya hewa ilinipendelea. Nilipata uzoefu mkubwa kutoka kwa kukimbia Birmingham na ndiyo iliyonisaidia hapa," alisema Kiplagat.

Kenya iliwakilishwa na vigogo watatu ambao wote walikosa kujishikia nafasi ya edali na kumaliza wa 7 na 14 / Picha : X World Athletics 

Medali ya fedha ilichukuliwa na Israel Maru Teferi aliyewakilisha Israel japo aliponea chupuchupu baada ya kuanguka na kujikmboa kilomita 30 kabla ya kumaliza. Alivuka mstari kwa kasi yake bora zaidi ya saa 2:09:12, Huku Muethiopia Leul Gebresilase akijitengea nafasi katika jukwaa kwa medali ya shaba kwa kasi ya saa 2:09:19.

Maru Teferi ambaye alizaliwa nchini Ethiopia na sasa anakimbilia Israel amesema kuwa alijitahidi kwani shindano hili lilikuw alengo kubwa sana kwake

''Nilianguka lakini haikunizuia...Nadhani kuna mtu alinigusa lakini nimefurahi nilifanikiwa kumaliza kwa medali katika hali nzuri zaidi'' aliongeza.

Kikosi cha Kenya hata hivyo kilichowakilishwa na vigogo watatu waliotarajiwa kumaliza angalau kwa medali waliambulia patupu huku Titus Kipruto akishikilia nafasi ya 7 kwa saa 2:10:47 na mwenzake Timothy Kiplagat akirushwa nyuma katika nafasi ya 14 kwa saa 2:11:25.

TRT Afrika