Bao la Uhispania lilipatikana dakika ya 29 kupitia kwa beki wa kushoto wa Real Madrid Olga Carmona./ Picha X FIFA Womenworldcup

Uhispania imekuwa timu ya tano ya kandanda ya wanawake kushinda Kombe la Dunia baada ya Marekani (mataji manne), Ujerumani (mataji mawili), Japan (taji moja) na Norway (taji moja).

Uhispania iliifunga England 1-0 katika muda wa kawaida na kushinda Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la 2023 kwenye Uwanja wa Australia Jumapili.

Bao la Uhispania lilipatikana dakika ya 29 kupitia kwa beki wa kushoto wa Real Madrid Olga Carmona.

Timu ya Uhispania ilitawala mpira katika kipindi cha kwanza, mara kwa mara wakiibana England kwenye nusu yao.

Mwaka wa 2015, timu hiyo ilibanduliwa kwenye mashindano katika hatua ya makundi. / Picha X FIFA WomensWcup

Kipindi cha kwanza ilikuwa bayana kuwa Uhispania ndio wenye kifua walipotawala 64% ya kumiliki mpira na kupiga mashuti zaidi langoni (matano) dhidi ya umiliki wa 36% wa England na mashuti matatu langoni.

Onyesho la ubingwa

Shambulio la Uhispania liliendelea katika kipindi cha pili. Timu hiyo ilipewa penalti dakika ya 70, lakini Jennifer Hermoso, aliyesonga mbele, alikosa kuendeleza uongozi wa Uhispania baada ya kipa wa England Mary Earps kuliziba shuti lake la chini lililoelekea lango la kulia.

Maguvu ya Uhispania yaliwasaidia kupata ushindi unaostahili, kwa kuonyesha ari katika kipindi cha pili na kuwashuhudia mabingwa hao wapya wakishinda angalau 55% ya umiliki wa mpira.

Kabla ya mashujaa wa 2023, Uhispania hapo awali ilishiriki Kombe la Dunia la Wanawake mnamo 2015 na 2019. Mwaka wa 2015, timu hiyo ilibanduliwa kwenye mashindano katika hatua ya makundi.

Mnamo 2019, Uhispania ilitolewa katika Kombe la Dunia la Wanawake katika Raundi ya 16 na washindi wa baadaye USA baada ya kufungwa 2-1.

TRT Afrika