Hii ni baada ya timu hiyo kupanda nafasi saba kutoka nambari 130 iliyokuwepo mwezi Aprili hadi nafasi ya123 ikiwa na jumla ya pointi 1138.79.
Haya yanatokana na msururu wa matokeo bora ya timu hiyo hivi karibuni ikiwemo kuifunga Niger 1-0 jijini Dar Es Salaam kwenye mechi ya hatua vya makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za komble la Afcon 2024. Ushindi huo uliipa Taifa Stars alama 3 muhimu na kupiga jeki matarajio yake ya kufuzu Afcon 2024 itakayochezwa nchini Cote D'Ivoire.
Licha ya Uganda kuteremka kutoka nafasi ya 89 hadi 92 ikiwa kutokana na fomu duni ya 'Korongo' hao, kulingana na jedwali hilo la FIFA, timu hiyo ndio inayoongoza katika mataifa bora Afrika Mashariki ikiwa katika nafasi ya 92, ikifuatwa na Kenya ilioko katika nambari 105.
Rwanda inashikilia nafasi ya 139, Burundi ikiwa katika nafasi ya 140, huku Ethiopia ikiwa katika nambari 143.
Sudan Kusini iko katika nafasi ya 168, Djibouti ikiwa katika nafasi ya193, Eritrea ikiwa katika nafasi ya198, huku Somalia ikishikilia mkia ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa katika nafasi ya 199.
Tanzania sasa inajiandaa kucheza na viongozi wa kundi F, Algeria, kwenye mechi za hatua ya makundi Afcon, zitakazopigwa tarehe 4 Septemba mwaka huu. Viwango vya ubora kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati - (CECAFA) kwa mujibu wa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani iliyotolewa na shirikisho la Soka duniani FIFA.