| Swahili
MICHEZO
1 DK KUSOMA
Tanzania: Klabu ya Simba yapata Afisa Mtendaji Mkuu mpya
Uwayezu Francois Regis, raia kutoka Rwanda anachukua nafasi ya Imani Kajula aliyejiuzulu nafasi hiyo miezi michache iliyopita.
Tanzania: Klabu ya Simba yapata Afisa Mtendaji Mkuu mpya
Uwayezu Francois Regis amewahi kuhudumu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya APR inayoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda./Picha: Wengine / Others

Miamba ya soka nchini Tanzania, Simba Sports Club imemtangaza Uwayezu Francois Regis kama Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu hiyo yenye maskani yake kwenye mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Regis, ambaye ni raia wa Rwanda amepata kuhudumu kama Makamu Mwenyekiti wa klabu ya APR FC inayoshiriki Ligi kuu ya Rwanda, anachukua nafasi ya Imani Kajula aliyejiuzulu miezi michache iliyopita.

Kupitia ukurasa wake Facebook, klabu hiyo imemtangaza Uwayezu kama mrithi wa Kajula aliyejiuzulu mwezi Julai, 2024.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji.

Kulingana na taarifa hiyom Regis anatarajiwa kuanza majukumu yake Agosti 4, 2024.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika