Bingwa wa Dunia kutoka Morocco Soufiane El Bakkali alimaliza wa kwanza kwa muda wa dakika 8:03.53 mbele ya Muethiopia Lamisha Girma (8:05.44) aliyetwaa medali ya fedha, na Mkenya Abraham Kibot aliyetwaa shaba (8:11.98).
El Bakkali ambaye hajawahi kupoteza mbio kubwa za kuruka viunzi tangu Septemba 2021
Mwanariadha huyo wa Morocco, alisema ameweka ushindi huo wa medali ya dhahabu siku ya Jumanne kwa niaba ya Mtukufu Mfalme Mohammed VI.
Soufiane El Bakkali
"Nina furaha sana kushinda taji hili la pili la dunia mfululizo." Ninatoa medali hii ya dhahabu inayoambatana na sherehe za watu wa Morocco katika Siku ya Vijana, kwa Mtukufu Mfalme 'Mohammed VI, Mwenyezi Mungu amlinde." Alisema.
Wakati huo huo, ushindi huo ulikuwa mtamu kwa El Bakkali, kwa kumpiku Muethiopia Lamesha Girma anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji.
“Nimeweza kushinda mbio hizi kutokana na mwongozo bora wa kocha wangu ambaye alinikumbusha mafanikio yangu ya awali, licha ya kukabiliana na mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia kwa tukio hili. Lamesha alijaribu kushika kasi katika mizunguko mitatu iliyopita, lakini nilizingatia kwa utulivu kiakili na kimwili kwa ajili ya ushindi,” mkimbiaji huyo wa Morocco aliongeza.
Soufiane El Bakkali, (27), ambaye ameshinda mbio zake zote tangu Septemba 2021, sasa ndiye mfalme asiyepingika wa mita 3000 baada ya kuweka kikomo utawala wa wakimbiaji wa Kenya na kuwa Mwafrika pekee mbali na Wakenya kushinda mbio hizo kwa muda mrefu.
Ushindi wa medali ya dhahabu wa El Bakkali umeifanya Morocco kuwa na medali 32 za dhahabu, 12 za fedha na 8 za shaba katika raundi mbalimbali za michuano ya Dunia.