Senegal wanacheza mechi yao ya 17 kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika - AFCON/ Picha CAF

Jumatatu Januari 15, ndio msema kweli kwa Senegal katika mashindano ya kombe la taifa biingwa Afrika AFCON. Kivumbi chote kitakuwa kutafuta kuhifadhi ubinwa wa kombe hilo kwa mechi yao ya kwanza ya makundi dhidi ya Gambia.

Simba ya Teranga na The Scorpions zinafungua rasmi kile ambacho kimechukuliwa kuwa Kundi la vifo katika Kundi C linalojumuisha pia Cameroon na Guinea.

Hakuna kitakachomridhisha kocha Alious Cisse na kikosi chake kilichojaa nyota ambacho kinatajwa kuwa mojawapo ya timu zinazopigiwa upatu kushinda na yenye vigogo wa kuogopewa kama vile Sadio Mane kwenye safu yao ya ushambuliaji.

Kumbuka Senegal watakuwa wanajribu kukwepa mkosi wa mabingwa wa kombe hilo, ambapo katika mashindano sita iliyopita, hakuna bingwa mtetezi aliyevuka awamu ya mchujo ya kumi na sita bora.

Japo ni timu inayoonekana kuwa wapya katika shindano hili, Gambia, ambao ni mara yao ya pili kushiriki wanajiamini kwani hata shindano lao la kwanza walipenya hadi robo fainali na kuwaacha wengi na butwaa.

Kocha wa Gambia, Tom Saintfiet alisema wanapania kufanya vyema katika mechi yao ya pili na wamejipanga vyema kwa ajili ya mashindano hayo.

"Tunafuraha kuwasili Côte d'Ivoire kwa mara ya pili mfululizo ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Tumejipanga vyema kwa mashindano hayo, na tuko tayari kwa ajili ya kuanza kwa mashindano,'' alisema kocha huyo. ''Tunatarajia fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Côte d "Ivoire kuwa maalum na nzuri, haswa kwa uwepo wa Gambia katika Kundi C pamoja na Senegal, Guinea na Cameroon,'' aliongeza.

Kipenga kinatarajiwa kuzua uchafuzi huo wa anga katika Uwanja wa Charles Konan Banny wa Yamoussoukro saa nane (14h00) kwa Saa za Côte d'Ivoire.

Kumbuka:

  • Hii itakuwa mechi ya kwanza kati ya Senegal na Gambia kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika la CAF.

  • Senegal na Gambia zilimenyana mara ya mwisho katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2010: michezo yote miwili ilimalizika kwa sare (0-0; 1-1).

  • Senegal wanacheza mechi yao ya 17 kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika - AFCON

  • Senegal wameshinda mechi yao ya ufunguzi katika kila moja kati ya nne zilizopita za Kombe la Mataifa ya Afrika la CAF

  • Hii ni mara ya pili kwa Gambia kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika la CAF.

  • Gambia walifika robo fainali katika ushiriki wao wa kwanza katika toleo la 2021, na hatimaye kufungwa 2-0 na Cameroon.

  • Licha ya kutinga robo fainali katika AFCON 2021, Gambia haijawahi kufunga zaidi ya bao moja katika mechi zao tano (W3 D1 L1). Ushindi wao wote watatu ulikuwa wa bao 1-0.

TRT Afrika