Gwiji huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid aliye na umri wa miaka 38, alionekana kutegwa na Soroush Rafiei ndani ya sanduku na muamuzi kutoka China Ma Ning akaelekeza kidole chake kwenye doa.
Ronaldo aliinuka ghafla na kumkaribia muamuzi, akionekana kutikisa kidole chake, na kichwa huku akimwambia hakukuwa na kosa.
Baada ya kutathmini mtambo wa var, muamuzi alishauriana na mwelekezaji wake na kubadilisha uamuzi wake kwenye mchuano huo wa makundi, kundi E, mjini Riyadh.
Hata hivyo, Ronaldo aliondoka mechi hiyo kutokana na jeraha la shingo kunako dakika ya 77, baada ya mlinda lango wa Persepolis Alireza Beiranvand kutua kwenye nyota huyo wa Ureno wakati wakiwania mpira wa juu.
Licha ya kutoka sare 0-0, matokeo hayo yalithibitika kutosha kwa Al Nassr kujihakikishia nafasi katika hatua za mtoano kama viongozi wa kundi.
Timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Pro nchini Saudia ililazimika kucheza muda mrefu mechini ikiwa na wachezaji 10 baada ya Ali Lajami kulishwa kadi nyekundu dakika ya 17.