Serikali ya Qatar imetoa vifaa vya michezo vilivyotumika katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022 kwa serikali ya Kenya.
Balozi wa Qatar nchini Kenya Mohammed bin Mutair Al Anazi aliikabidhi Kenya vifaa hivyo vya michezo kwa mwakilishi wa serikali ya Kenya kule bandari ya Mombasa.
Kombe la Dunia La FIFA Qatar 2022, lililobebwa na Argentina, liliashiria hatua muhimu katika historia ya Qatar na dunia zima ya Kiarabu.
Shindano hilo pia liliacha urithi wa kijamii, kibinadamu, kiuchumi na mazingira kwa nchi hiyo na eneo nzima.
Vifaa hivyo vinatarajiwa kupiga jeki sekta ya michezo nchini Kenya huku taifa hilo likizidi kujiandaa kuwa mwenyeji wa Kombe la Afcon, pamoja na Uganda na Tanzania, maarufu Pamoja 2027.
TRT Afrika