Wasanii wa Drag Queen wanaojishabihisha na wanawake wameshutumiwa kudhihaki imani ya Kikristu na kanisa hilo. / Picha : Reuters 

Mchezo wa kuigiza mlo wa Mwisho wa Yesu na wafuasi wake, wakati wa sherehe ya Ijumaa ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris ya 2024 ulizua taharuki, ikiwemo kutok akwa Askofu wa kanisa Katoliki Robert Barron wa Minnesota.

Kikundi cha Drag Queens, yaani wanaume waliovalia kike na mapapmbo ya kupitiliza waliigiza mchoro wa kisanii wa Leonardo da Vinci wa Mlo wa Mwisho wa Jioni, mlo wa mwisho wa Yesu Kristo pamoja na wanafunzi wake.

Katika chapisho la video kwenye X, Barron alisema kitendo hicho kilikuwa ishara ya "jamii ya kidunia ya kisasa" ambayo inatambua Ukristo kama adui yake.

Akirejelea kumbukumbu yake ya anavyoupenda mji wa Paris, ambapo alisomea kwa miaka mitatu, Barron aliikosoa Ufaransa kwa "dhihaka mbaya."

Alihoji kwa nini Ufaransa, ambayo imetuma wamishonari wa Kikatoliki duniani kote na ambao utamaduni wao wa "kuheshimu mtu binafsi na haki za binadamu na uhuru" licha ya kujikita sana katika Ukristo, ilichagua "kukejeli imani ya Kikristo."

Aliwasihi Wakristo na Wakatoliki wasiwe wavivu, bali wafanye "sauti zao zisikike."

AA