Olimpiki: FIFA yakataa malalamiko ya Argentina ya VAR dhidi ya Morocco

Olimpiki: FIFA yakataa malalamiko ya Argentina ya VAR dhidi ya Morocco

Argentina ilipoteza mechi ya Jumatano kwa kufungwa mabao 2-1 na Morocco.
Cristian Medina wa Argentina akicheza na Zakaria El Ouahdi wa Morocco. Picha / Reuters

Shirikisho la Soka Duniani FIFA, limekataa malalamiko ya Argentina kuhusu kusawazisha bao la dakika za mwisho katika mechi ya ufunguzi ya Olimpiki ya Majira ya joto dhidi ya Morocco, mkuu wa chama cha soka cha Argentina (AFA) alisema Jumamosi.

"Kamati ya Nidhamu ya FIFA ilikataa malalamiko yaliyowasilishwa kuhusiana na matukio yaliyotokea katika mechi dhidi ya Morocco," Rais wa AFA Claudio "Chiqui" Tapia alisema kwenye X, akisema anatafuta maelezo ya uamuzi huo.

Argentina ilipoteza mechi ya Jumatano, mchezo wa ufunguzi wa kandanda kwa wanaume wa Olimpiki ya Paris, kwa matokeo ya mwisho ya 2-1 dhidi ya Morocco.

Awali mechi hiyo ilisitishwa kwa sare ya 2-2 huku kundi la mashabiki likiingia uwanjani, na saa mbili baadaye mwamuzi msaidizi wa video (VAR) alikataa bao la mwisho la Argentina.

Uvamizi wa mashabiki

Waandalizi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris walisema Alhamisi walikuwa wanafanya kazi kubaini kilichosababisha mashabiki hao kuingia uwanjani.

"Katika kutetea haki zetu, AFA itauliza kwa misingi gani uamuzi huo ulifanywa na kutathmini rufaa husika," Tapia alisema.

Soka inaongoza kwa wafuasi wengi nchini Argentina, ambayo imepata ushindi mara tatu wa Kombe la Dunia - wa hivi punde dhidi ya Ufaransa mnamo 2022.

Argentina pia ilishinda ligi kuu ya bara la Amerika mapema mwezi huu, kwa kuwashinda Colombia katika fainali nyingine yenye machafuko huko Miami na kuandikisha ushindi wa 16 wa rekodi ya Copa America.

TRT Afrika