Nchi saba tayari zimejikatia tikiti kwa kufuzu kwenye mashindano ya UEFA EURO 2024 msimu ujao wa joto nchini Ujerumani.
Huku mbio za kusaka tiketi za mataifa mbalimbali zikiendelea, jumla ya timu saba zimejihakikishia nafasi kwenye ngarambe hizo.
Austria iliizaba Azerbaijan jumatatu tarehe 16 Oktoba na kuhakikisha wamefuzu kutoka kundi F wakiwa pamoja na Ubelgiji. Austria imefika EURO yao ya tatu mfululizo na ya nne kwa jumla; baada ya kushirikiana na mashindano ya 2008 na majirani Uswisi.
Ubelgiji iliwanyuka wapinzani wao wakuu wa Kundi F Austria kwa mabao 3-2 mnamo Oktoba 13 ili kujinyakulia nafasi katika EURO yao ya tatu mfululizo kwenye kampeni yao ya kwanza chini ya kocha Domenico Tedesco.
Washindi mara mbili Ufaransa, walitinga michuano ya Ujerumani 2024 baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Uholanzi mnamo Oktoba 13.
Les Bleus wa Ufaransa hawajawahi kukosa fainali za UEFA EURO tangu 1988.
Ufaransa, chini ya kocha Didier Deschamps tangu 2012, walikuwa wenyeji wa mwaka 2016, walipoteza dhidi ya Ureno katika fainali.
Ureno ilifuzu baada ya kuwashinda wapinzani wao wa Kundi J Slovakia 3-2 mnamo Oktoba 13 ili na kutua fainali yao ya kwanza chini ya kocha mpya Roberto Martínez.
Nyota wa timu Hiyo, Cristiano Ronaldo, ambaye anashikilia rekodi ya mabao mengi (14) na kushiriki mara (25) kwenye mashindano hayo, atafuzu kwa makala yake ya sita ya fainali za EURO nchini Ujerumani ikiwa ataitwa kikosini.
Uturuki ilifuzu kwenye fainali yao ya tatu mfululizo ya EURO baada ya kupata ushindi wa 4-0 nyumbani kwao dhidi ya Latvia mnamo Oktoba 15.
Uhispania, walihitimu kwa kombe la Euro kwa mara ya 12 katika mashindano hayo baada ya kuishinda Norway 1-0 mjini Oslo tarehe 15 Oktoba.
Scotland inayoongozwa na kocha Steve Clarke, ilithibitishwa kama washiriki wa fainali za Ujerumani baada ya Norway kushindwa kupata alama tatu nyumbani dhidi ya Uhispania mnamo Oktoba 15.