Wachezaji wa Yanga SC mazoezini | Picha: Twitter Yanga

Mchezo unatarajiwa kuchezwa mida ya saa moja 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Utaratibu mpya wa ngao ya hisani

Ngao ya hisani kwa mwaka huu wa 2023/2024 itachezwa kwa sura tofati na ilivyozoeleka.

Timu 4 zitashiriki, washindi wa mechi za kwanza watakutana kwenye mechi ya fainali na mshindi atanyakua kikombe cha hisani. Na waliopoteza mechi za kwanza watakutana kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.

Wachezaji wa kigeni hati hati kukosa michezo

Joto la mechi likiendelea kupanda, mapema hii leo Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya maandishi inayosema ni timu ya Azam FC pekee ndiyo imewasilisha vibali vya wachezaji 10 wa kigeni.

Wachezaji wa Azam mazoezini | Picha: Twitter Azam FC

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wachezaji wa kigeni wa timu za Simba SC, Singida Fountain Gate na Yanga SC hawatoruhusiwa kucheza michezo ya ngao ya hisani mpaka taratibu za kisheria zitakapokamilishwa na timu zao.

TRT Afrika