Martin Bakole / Photo: AFP

Kwenye pambano la ndondi lililofanyika Aprili 22, 2023 huko Rzeszow, Poland, bondia wa Congo, Martin Bakole aibuka mshindi dhidi ya mpinzani wa Ukreni, Igor Shevadzuktskiy, akishinda kwa K.O kwenye raundi ya tatu.

Wakati wa pambano hilo, mpiganaji huyo wa Kiukreni alivumilia kupigwa mara kwa mara, na hatimaye kupoteza fahamu katika raundi ya tatu.

Martin Bakole ameweza ibuka mshindi kwenye mapambano 19 kati ya 20 ikiwemo ushindi 15 kwa mtoano (K.O), ushindi 4 kwa uwazi na kupoteza mapambano moja kwa mtoano (K.O).

Kwenye mtandao wake wa kijamii, Martin Bakole ali shukuru raia wote wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa kumuunga mkono na kuahidi kwendelea kuwakilisha DRC popote ulimwengu.

''Raia wa Congo wanajivunia wewe, wewe ni kioo cha jamii - Ahsante kupepea bendera ya Congo huko Poland'' aliisema Kabulo mwana Kabulo, Waziri wa Michezo na Burudani Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

TRT Afrika