Mikwaju 34 za penalti zaamua mshindi mechini Misri, kati ya Modern Future na Pyramids

Mikwaju 34 za penalti zaamua mshindi mechini Misri, kati ya Modern Future na Pyramids

Modern Future ilishinda Pyramids na kujihakikishia nafasi yao katika fainali ya Kombe la Super la Misri.
Al Ahly itachuana na Modern Future kwenye fainali  / Picha: Reuters

Baada ya mshindi kukosekana katika muda wa kawaida wa mchezo huo uliomalizika bila bao lolote, ilibidi mshindi asakwe kupitia penalti.

Aidha, timu hizo ziliweka historia kwenye mikwaju ya penalti kwani timu zote mbili ziliweka rekodi mpya ya kila upande kupiga jumla ya mikwaju 17.

Modern Future FC walijihakikisha nafasi yao katika fainali kwa kuifunga Pyramids FC 14-13 kupitia mikwaju ya penalti katika mechi iliyochezwa uwanja wa Mohammed Bin Zayed UAE.

Fainali ya kukata na shoka inasubiriwa mnamo Ahamisi hii, ambapo Modern Future FC itakabiliana na Al Ahly, mshindi wa pambano la pili la nusu fainali ya pili kwa kuifunga Ceramica Cleopatra, siku ya Jumatatu.

Beki wa Pyramids Osama Galal alipoteza penalti mbili, ikiwemo moja ambayo ilipa ushindi Modern Future FC.

Ingawa kuna kipindi mashabiki walihisi kuwa mikwaju hiyo haingemalizika, ilikuwa chache mno ikilinganishwa na mikwaju 54 iliyopigwa kuipa ushindi Washington FC iliyoipiga Bedlington Terriers 25-24 nchini England mnamo 2022.

Aidha, mnamo 2005, mechi ya Kombe la Namibia kati ya KK Palace na Civics ilishuhudia penalti 48.

TRT Afrika na mashirika ya habari