Mshambulizi wa zamani wa Japan Kazuyoshi Miura aliongeza rekodi yengine katika maisha yake ya kukiuka umri, na kucheza kwa mara ya kwanza katika klabu ya daraja la pili ya Ureno ya Oliveirense akiwa na umri wa miaka 56.
Miura, ambaye alijiunga na Oliveirense kwa mkopo kutoka Yokohama FC mapema mwaka huu, aliingia uwanjani dakika ya 90 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Academico de Viseu Jumamosi.
Miura, ambaye yuko katika msimu wake wa 38 wa soka la kulipwa, amechezea msururu wa vilabu kote ulimwenguni vikiwemo Palmeiras, Genoa, Dinamo Zagreb na Vissel Kobe.
Ureno ni nchi ya sita kwa Miura, ambaye amebatizwa jina la "King Kazu" na mashabiki, baada ya kuanza maisha yake ya kuzunguka-zunguka kwa kuinoa Santos ya Brazil mnamo 1986.
Aliichezea Japan mara 89, akishinda Kombe la Asia mnamo 1992, na ndiye mfungaji bora wa pili wa muda wote wa nchi hiyo akiwa na mabao 55. Mechi yake ya mwisho ya kimataifa ilikuwa mwaka 2000.