Sifaan Hassan an Faith Kipyegon watapambana na Bingwa wa sasa wa mita 5000  Gudaf Tsegay wa Ethiopia/ Picha : Reuters 

Wasimamizi wa mashindano ya riadha ya dunia yanayofanyika mjini Budapest Hungary, wamesimamisha mbio za mchujo za wanawake za mita 5000 kutokana na hali mbaya ya hewa ikiwa joto limepanda zaidi ya nyusi 32.

Shirikisho la Riadha, World Athletics lilisema katika taarifa yake kwamba joto la Wet Bulb Globe (WBGT) - ambalo linatokana na mchanganyiko wa mambo ikiwa ni pamoja na halijoto ya hewa, unyevunyevu, mwelekeo wa upepo na uwepo wa mawingu ya mvua - haitakuwa katika kiwango kinachokubalika kwa wanariadha.

''Kupanda kwa joto huko Budapest kumetulazimu kuzuia kwa muda mbio za wanawake za mita 5,000 kutoka kipindi cha asubuhi hadi kikao cha jioni Jumatano,'' World Athletics ilisema, na kuongeza kuwa ''...mbio za mita 200 kwa wanaume na wanawake zitaanza mapema Jumatano.''

Gudaf Tsegay wa Ethiopia ndiye bingwa wa dunia mtetezi wa mbio za mita 5,000. Jitihada zake za kuhifadhi taji hilo zitamfanya akabiliane na Mkenya Faith Kipyegon - anayeshikilia rekodi ya dunia kwa kitengo hicho.

Reuters
TRT Afrika