Police tape secures a crime scene outside a club after a shooting in Brooklyn on October 12, 2019. / Photo: AFP

Rubayita, mkimbiaji wa mbio za masafa marefu kutoka Rwanda, mwenye umri wa miaka 34, alikumbana na mauti huko kambi maarufu ya wanariadha ya Iten, bonde la Ufa, Kenya, kwenye hali ya kutatanisha ikihusisha mahusiano yenye mapenzi na wivu.

Mkimbiaji huyo alikuwa anaishi katika kambi maarufu ya mazoezi ya Asic, Iten, tangu 2017, huku akifanya bidii na kujitolea ili kuiwakilisha Rwanda kwenye majukwaa ya kimataifa pamoja na kufuatilia matamanio yake ya riadha.

Hata hivyo, kulingana na rafiki zake, Rubayita alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Nelvin Ajuma, mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Tiba cha Kenya (KMTC) mwenye umri wa miaka 28.

Rubayita, alikutana na kifo chake siku moja tu kabla ya kuondoka Kenya kuelekea nchini Kampala, Uganda, kesho yake asubuhi ambako alipaswa kuchukua viza yake ya Italia. Alipakia mabegi yake tayari kushiriki katika mbio za marathon nchini Italia.

Kulingana na Tom Makori, kamanda wa polisi eneo la tukio, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba Khamala, alisababisha ugomvi mkali kati yake na Rubayati na kumuacha Rubayita akiwa amelala kando ya barabara akiwa na majeraha kichwani na mdomoni, na kuvuja damu kwenye sikio lake la kushoto.

Taarifa za polisi zinathibitisha kuwa Ajuma na Rubayita, ambao zamani walikuwa wapenzi, walikuwa kwenye mchakato wa maridhiano, jambo ambalo Khamala alikataa.

Maafisa wa upelelezi nchini Kenya wamefanikiwa kumkamata Duncan Khamala, mwanariadha mwenye umri wa miaka 27 wa mbio fupi na anakimbia mita 100 na 200, ambaye anashukiwa kuhusika kwenye mauaji ya Rubayita akiwa mshukiwa mkuu pamoja na pamoja na mwanamke mmoja anayeaminika kuwa kiini cha mzozo huo unaodaiwa kusababisha kifo cha Rubayita.

Juhudi za utekelezaji wa sheria zimeongezeka katika jitihada zao za kumkamata Duncan Khamala, mwanariadha mwenye umri wa miaka 27 ambaye anashukiwa kuhusishwa na mauaji ya Rubayita.

Familia ya mwanariadha huyo wa Rwanda Siraj Rubayita, kimelaani kifo chake na "kitendo kisicho na maana cha vurugu" kilichosababisha mauaji ya mwanao.

"Katika kipindi hiki kigumu, tunaomba uvumilivu na uelewa tunapopitia changamoto zilizo mbele yetu. Lengo letu linabaki katika kumuomboleza mtoto wetu na kutoa ushirikiano kamili kwa mamlaka katika kutafuta ukweli na haki,” iliendelea.

Shirikisho la Riadha la Rwanda (RAF) kupitia Katibu Mkuu wake Jean Paul Niyintunze, imetoa taarifa ya kusikitishwa na mauaji ya mwanariadha huyo.

"RAF limepata, kwa masikitiko makubwa, habari kuhusu kifo cha Rubayita Siraj Mwanariadha wa zamani wa Masafa ya Kati na Marefu aliyefariki Kenya ambako amekuwa akifanya mazoezi." Iliandika.

"Kwa niaba ya Familia ya wanariadha tunatoa pole kwa familia yake na familia nzima ya wanariadha kwa msiba huu usioweza kufidiwa. Mawazo na maombi yetu yako pamoja nanyi." Ilisema.

Kwa sasa, Mwili wa Rubayite, umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Iten ukisubiri uchunguzi.

TRT Afrika