Timu hizo zitakutana kwa mara ya kwanza Februari 11, 2025 jijini Manchester kabla ya kurudiana tena Februari 18, jijini Madrid./Picha: Wengine

Manchester City na Real Madrid, zinakutana tena katika hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), baada ya droo iliyofanyika Januari 31 nchini Uswisi.

Timu hizo zitakutana kwa mara ya kwanza Februari 11, 2025 jijini Manchester kabla ya kurudiana tena Februari 18, jijini Madrid.

Kabla ya hapo, timu hizo zimewahi kukutana mara tano katika hatua hiyo ndani ya miaka tisa, huku Real Madrid ikiibuka na ushindi, isipokuwa katika msimu wa 2022/23 kwenye hatua ya nusu fainali, ambapo Manchester City ilikwenda kubeba kombe hilo kwa mara ya kwanza kabisa.

Katika matokeo mengine ya droo hiyo iliyopangwa katika makao makuu ya UEFA jijini Nyon, Uswisi Brest ya nchini Ufaransa itachuana na Paris Saint-Germain, huku Club Brugge ya Ubelgiji itakuwa mwenyeji wa Atalanta ya nchini Italia.

Juventus ya Italia, maarufu kama ‘kibibi kizee cha Turin’, imepangwa na PSV Eindhoven ya Uholanzi wakati Sporting ya Ureno itachuana na Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Monaco ya Ufaransa imepangwa kukutana na Benfica ya Ureno huku Celtic ya Scotland ikiwa mwenyeji wa FC Bayern Munich ya Ujerumani.

Mechi zote zitachezwa kati ya Februari 11 na 12, 2025 na kurudiwa tena Februari 18 na 19, 2025./Picha: Wengine

Kulingana na droo hiyo, Feyenoord ya Uholanzi imepangwa kuanza na AC Milan ya nchini Italia.

Mechi zote zitachezwa kati ya Februari 11 na 12, 2025 na kurudiwa tena Februari 18 na 19, 2025.

TRT Afrika