Raia wa Liberia wamepiga kura Jumanne kuamua kati ya nyota wa zamani wa soka George Weah anayesaka muhula wa pili dhidi ya mwanasiasa mkongwe na makamu wa rais wa zamani Joseph Boakai. Picha: Getty

George Weah ni mwanasoka wa kwanza Afrika kuwa rais, baada ya kustaafu kutoka soka mwaka 2002.

George Weah alichaguliwa rais wa Liberia mnamo 2018, baada ya kupoteza uchaguzi wake wa kwanza wa urais nchini Liberia mnamo 2005.

Nyota huyo mstaafu, ni mwanaspoti wa kwanza wa kimataifa wa Liberia kuchaguliwa kuingia bungeni alipochaguliwa kuwa Seneta mnamo 2014.

George Weah ni mchezaji wa kwanza na pekee wa Afrika hadi leo kushinda tuzo maarufu ya Ballon D'or, pamoja na tuzo ya mwanasoka bora duniani, FIFA aliposhinda 1995.

Aidha, Weah pia ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka barani Afrika 1989, 1994 na 1995.

Mnamo 1995, alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya akiichezea PSG.

Amewakilisha timu za As Monaco, Olympique Marseille na PSG za Ufaransa, Ac Milan ya Italia, Chelsea na Manchester City za Uingereza.

Weah ana kipaji cha kuimba. Ameshiriki wimbo, Lively Up Africa, wimbo wa kukusanya fedha kwa ajili ya watoto. Weah alirekodi na kutoa muziki wa kuhamasisha dhidi ya Eola na COVID kama rais.

George Weah, alikua balozi wa kujitolea wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF.

Mwaka 2011 alihitimu na shahada ya usimamizi wa biashara kutoka Chuo Kikuu Cha DeVry Huko Florida.

TRT Afrika na mashirika ya habari