Mohamed Salah. Picha:Wengine 

Salah alipata fursa hiyo baada ya kufunga goli la kwanza kwenye mechi yao dhidi ya Lille usiku ya Jumanne. Liverpool ilipata ushindi wa 2-1.

Kwa ushindi huo sasa Liverpool imeshinda mechi zake zote saba na iko kileleni mwa jedwali la msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 21. Imebaki mechi moja kukamilisha mzunguko wa kwanza wa mechi hizo.

Kwa matokeo hayo sasa Salah amefunga magoli 20 katika Ligi ya Klabu barani Ulaya akiwa katika uwanja wa nyumbani wa Anfield, na amepata jumla ya mabao 44, na magoli matano katika Ligi ya Europa msimu uliyopita, huku goli moja akilipata katika hatua ya kuwania kufuzu kwa ligi hiyo.

Inamuweka kwenye safu moja na wachezaji wengine mashuhuri kama vile Sergio Aguero na Ruud van Nistelrooy. Wachezaji hao waliwahi kufunga magoli mengi kwenye ligi ya Klabu bingwa katika uwanja mmoja wakichezea vilabu vya ligi kuu ya England.

Kwa mafanikio hayo, kocha wa Liverpool Arne Slot alimuelezea Mohamed Salah kama mshambuliaji ''hodari''.

TRT Afrika