Ligi ya Mabingwa kwa wanawake CAF 2023 yaanza Cote D'ivoire. Picha: CAF

Ligi ya Mabingwa ya Wanawake CAF imeng'oa nanga nchini Ivory Coast Jumapili tarehe 5 Novemba katika uwanja mpya wa Amadou Gon Coulibaly, Korhogo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika Afrika Magharibi.

Dimba hilo lilifunguliwa kwa mechi kati ya wenyeji, Athletico Abidjan ni klabu ya kwanza ya wanawake kutoka Cote D'ivoire kucheza katika fainali za ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF ikichuana na SC Casablanca kutoka Morocco.

Mechi hiyo iliishia sare ya 1-1 huku Espérance Agbo akifunga bao la kwanza kabisa katika uwanja wa Amadou Gon Coulibaly Athlético D'abidjan ikitoka sare 1-1 na Sporting Club Casablanca katika mechi ya ufunguzi wa Ligi ya mabingwa ya wanawake ya CAF jumapili.

N'Guessan Nadège Koffi aliisawazishia Sporting Club Casablanca kwenye droo hiyo.

Aidha, mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns waliifunga JKT Queens ya Tanzania 2-0 kwenye mechi ya pili ya siku ya Jumapili.

Kulingana na ratiba ya leo, Huracanes FC kutoka G. Equatorial, ilichuana na AS Mande ya Mali Ugani Laurent Pokou huku mabingwa wa zamani ASFAR Club ikikwaruzana na Ampem Darkoa Ladies F.C. mechi ya pili na ya mwisho siku ya Jumatatu.

Kundi A: Athletico Abidjan (Côte D'ivoire), SC Casablanca (Moroko), JKT Queens (Tanzania), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

Kundi B: Huracanes FC (G. Equatorial), AS FAR Moroko, AS Mande (Mali), Ampem Darkoa FC ya (Ghana).

Klabu zinazoshiriki ni pamoja na washindi wawili wa awali: ASFAR kutoka Moroko na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Ligi hiyo ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF inaashiria wakati wa kusisimua kwa Taifa La Ivory coast kwani itawapa Caf na Kamati ya maandalizi ya ndani mazingira bora ya kutathmini hali yake ya utayari kabla ya kombe la mataifa ya Afrika ya Caf.

TRT Afrika