Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Tunisia Faouzi Benzarti./Picha: Wengine

Tunisia imemtimua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Faouzi Benzarti baada ya kupoteza mchezo wao na visiwa vya Comoro, Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema siku ya Jumanne.

Benzarti, mwenye umri wa miaka 74, aliiongoza Tunisia kushika usukani wa kundi A kwenye michezo ya kufuzu AFCON 2025, licha ya kupoteza na baadaye kutoka suluhu ya 1-1 na timu ya taifa ya Comoro.

Benzarti alipewa mikoba ya timu ya taifa ya Tunisia mwezi Septemba, wakati wa michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2025), ambapo aliiongoza timu hiyo kushinda michezo miwili dhidi ya Madagascar na Gambia.

Kabla ya hapo, Benzarti aliwahi pia kuwa mkufunzi wa Tunisia kwa vipindi vitatu, yaani kwa mwaka 1994, 2010 na 2018 mtawalia.

Fainali za AFCON 2025, zitafanyika nchini Morocco kuanzia Disemba 2, 2025 hadi Januari 18, 2026.

TRT Afrika