Uwanja huu wa Kasarani, pia umefungwa kwa matumizi ili kufanyiwa ukarabati baada ya kutumika muda mrefu. Picha: Getty

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa Joe Kadenge, uliojulikana kuwa uwanja wa zamani Uwanja wa Jiji la Nairobi zimefanyika leo.

Uwanja huo utakuwa wa kiwango cha FIFA, na kuwa na uwezo wa kuwalaki mashabiki 10,000 pamoja na kuandaa mbio za riadha.

Uwanja huo pia utakuwa na taa za kuwezesha mechi za soka kuchezwa usiku, vyumba vya kubadilishia nguo, kituo cha mazoezi, mkahawa, ofisi, sehemu ya kuegesha magari ya hadi magari 100 miongoni mwa uwezo mbalimbali.

Hapo awali, uga huo ulikuwa uwanja wa nyumbani wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia, huku ukiwaingiza mashabiki 10,000 kabla ya kufungwa kwa ukarabati hapo awali na kutotumika kwa zaidi ya miaka mitatu.

Uwanja wa 'Joe Kadenge', yaani City, ndio uwanja kongwe zaidi wa michezo jijini Nairobi kwani ulijengwa mwanzoni mwa miaka ya 1960 hata kabla ya Kasarani na Nyayo na kuandaa hafla mbalimbali za kihistoria.

TRT Afrika