Kenya: Mwanariadha Rodgers Kwemoi afungiwa miaka sita

Kenya: Mwanariadha Rodgers Kwemoi afungiwa miaka sita

Hii ni baada ya kuhusishwa na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.
Taasisi ya  Athletics Integrity United imemtia Rodgers Kwemoi kwa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu./Picha:Getty

Taasisi inayochunguza mienendo ya wanariadha duniani ya Athletics Integrity United (AIU) imemfungia kwa miaka sita, mwanariadha Rodgers Kwemoi huku ikiainisha matendo 18 yanayohusisha tuhuma za kutumia madawa ya kusisimua misuli.

Mengi ya matukio hayo yalifanyika kuanzia Julai 2016 hadi Septemba 2022, kabla ya mashindano makubwa, kulingana na taasisi hiyo.

Kwemoi anakumbukwa kwa uhodari katika mbio za mita 10,000 katika michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 2018 ambapo alitwaa medali ya shaba na pia kumaliza nafasi ya nne katika mashindano ya ubingwa wa dunia ya mwaka 2019.

TRT Afrika