Bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu Anthony Joshua alimshinda Mfini Robert Helenius kwa mtoano wa raundi ya saba kwa ngumi moja na kujiweka sawa kukutana na Mmarekani Deontay Wilder mwaka ujao.
Helenius, akipigana badala ya Muingereza Dillian Whyte aliyeondolewa kwenye pambano lisilo la ubingwa kwa kukutwa na hatia ya kutumia dawa zilizoharamishwa wiki moja iliyopita, alidumu kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa lakini alianguka kwenye turubai dakika moja na sekunde 27 kwenye raundi ya Jumamosi.
Baadhi ya umati wa watu katika ukukmbi wa 02 mjini London, ambao walikuwa wamekosa utulivu na hata kuanza kumzomea Joshua kwa kukosa kufunga kazo raundi ya tatu , walikuwa wakielekea kutoka wakati huo mara wakashtukizwa na fataki moja kali iliyomweka chini Helenius.
Joshua alionekana kusitasita mwanzoni na kujizuia au kuonekana kama hayuko fomu sawa wakati Helenius, ambaye alipigana nchini Finland wiki moja tu iliyopita, alionekana kuwa mkaidi na imara kabisa tayari kunyakua ushindi.
Umati wakosa subira
Aliondoka mara moja kutoka kwenye ring bila kusema neno moja, punde tu muamiuzi aliposimamisha pigano.
Kisha aligoteana na mashabiki kadhaa na kuonja kinyuaji cha bingwa wa zamani wa UFC Conor McGregor kabla ya kurudi ndani ya riung
Helenius alipokea matibabu na oksijeni kabla ya kuweza kusixmama tena.
“Nilijua hili lingetokea, kila mtu anazungumza kuhusu AJ mpya na AJ wa zamani na baada ya raundi mbili au tatu watu wanaanza kukosa subira,” mmoja wa wasimamizi wa Joshua, Eddie Hearn aliambia vyombo vya habari.
Huu ni ushindi wa Knock out wa 23 wa Joshua, kufikisha rekodi yake ya kushinda mara 26 na kushindwa mara tatu, lakini rekodi yake ya kwanza tangu Desemba 2020 alipomshinda Mbulgaria Kubrat Pulev katika kutetea ubingwa wa WBA, IBO, IBF na WBO jijini London.
Kumekuwa na gumzo kuhusu Joshua kupigana na Wilder, bingwa wa zamani wa WBC, mwaka ujao lakini Muingereza huyo anahitaji kuendelea kushinda ili kuzungumziwa katika pumzi sawa na bingwa wa Marekani na bingwa mtetezi Tyson Fury.