Michezo hiyo imepangwa kufanyika Septemba 4 na 12, 2024, ambayo itakuwa wakati wa mapumziko ya kimataifa ya FIFA/ Picha: Reuters 

Na Kevin Philips Momanyi

TRT Afrika, istanbul

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars inatarajiwa kumenyana na wababe wa soka duniani Uhispania na Brazil katika mechi za kirafiki.

Michezo hiyo imepangwa kufanyika Septemba 4 na 12, 2024, ambayo itakuwa wakati wa mapumziko ya kimataifa ya FIFA.

Kenya itacheza na Uhispania mnamo Septemba 4 kwenye Uwanja wa Real Madrid, Santiago Bernabeu, na Brazil mnamo Septemba 12 kwenye uwanja huo huo.

Kocha mkuu wa Kenya Engin Firat wa Uturuki amelitaka shirikisho la kandanda nchini kenya (FKF) kupanga mechi na timu zilizoorodheshwa zaidi ya Harambee Stars tangu alipochukua nafasi hiyo.

Shirikisho la Soka la Kenya linasema kuwa michezo hiyo itawapa Harambee Stars uzoefu unaohitajika na kwa mechi zijazo za maandalizi Harambee Stars walikuwa Malawi kwa mapumziko ya hivi majuzi ya Machi 2024 ya kimataifa.

Walicheza na Zimbabwe na wenyeji, wakishinda kombe la Mataifa manne-ushindi wa kwanza kuu wa Firat kama kocha mkuu.

Mnamo 2023, Kenya ilicheza na Iran, Qatar na Urusi.

TRT Afrika