Klabu ya Galatasaray ya Uturuki itakutana na Molde siku ya Jumanne kwenye mchuano wa mkondo wa pili kufuzu kwa hatua ya makundi ya UEFA Champions League.
Galatasaray inaingia mechi hiyo kifua mbele kufuatia ushindi wake wa 3-2 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya wageni wake wa leo kutoka Norway Molde, kufuatia bao la Fredrik Midtsjo.
Pambano la leo la marudiano litagaragazwa katika uwanja wa Ali Sami Yeni Sports Complex mjini Istanbul.
"Tuko nyumbani, na tutacheza kutumia fursa hiyo. Kwa msaada wa mashabiki wetu tunataka kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa." Okan Buruk, kocha wa Galatasaray amesema.
"Tunajaribu kuwa timu ambayo ni ngumu kufungwa, na natumai itakuwa hivyo hapa. Natumai haitokuwa siku ya Icardi. Hatujaweka hatua maalum za kukabiliana naye. Ikiwa tutashikamana na mipango yetu, tunaweza kufikia matokeo tunayotaka." Kocha wa Molde, Erling Moe amesema.
Szymon Marciniak kutoka Poland ametajwa kuwa refa wa mechi hiyo.