Alfajiri bado haijatoweka katika nyanda za juu za Bonde la Ufa la Kenya wakati nyota wa mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge akijinoa katika kambi yake ya mafunzo.
Eliud Kipchoge anajiandaa kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki katika kambi ya mazoezi ya Kaptagat akiwa pamoja na nyota wa masafa ya kati wa Kenya Faith Kipyegon pamoja na wakimbiaji wa ndani wanaokuja kwa matumaini ya vipaji vyao kutambulika.
"Kila kitu kinaendelea vizuri. Ninajihisi vizuri. Lakini nadhani miezi ijayo itakuwa ya kuvutia zaidi, " Kipchoge anaiambia AFP katika mahojiano baada ya mazoezi.
Kufikia sasa, Kipchoge, ni mmoja wa wakimbiaji watatu pekee wa mbio za masafa marefu wenye mataji mawili ya Olimpiki (2016, 2021), pamoja na Abebe Bikila Wa Ethiopia (1960, 1964) na Waldemar Cierpinski wa Ujerumani (1976, 1980).
"Michezo ya Olimpiki ni muhimu kwangu," Kipchoge anasema.
Maandalizi ya Kipchoge pia yanahusisha juhudi za kupambana na dawa za kulevya, ambazo zimeimarishwa na shirikisho la riadha la Kenya chini ya shinikizo kutoka kwa mamlaka ya kimataifa.
"Paris ni eneo ambalo maisha yangu yalianza katika riadha miaka 20 iliyopita."
Lakini kurejea kwake katika mji mkuu wa Ufaransa ni ishara ya fahari. Ilikuwa hapo ambapo mnamo 2003, akiwa na umri wa miaka 18, alishinda taji lake la kwanza la kimataifa: kwa kuwa bingwa wa dunia wa mita 5,000 mbele ya magwiji wawili, Hicham El Guerrouj wa Moroko na Kenenisa Bekele wa Ethiopia.
Malengo yake yanabaki imara licha ya maonyesho mawili duni ya hivi karibuni, huko Boston mnamo 2023 wakati alimaliza wa sita na, na Tokyo mnamo Machi ambapo alimaliza tu wa 10 -- kuvutia ukosoaji na shaka juu ya maisha yake ya baadaye.
Ingawa siku zinazidi kuelekea kile kinachoweza kuwa Olimpiki yake ya mwisho, lakini Kipchoge hataki kuzungumza juu ya hilo: "ninachukua hatua moja kwa wakati wake."
Bingwa huyo wa zamani wa rekodi mbili za dunia yuko katika hatua za mwisho za maandalizi ambayo itamwongoza kutimiza lengo la kihistoria -- kuwa mtu wa kwanza kutwaa dhahabu ya Olimpiki ya Marathon mara tatu mfululizo.