Copa del Rey - Final - Real Madrid v Osasuna / Photo: Reuters

Rodrygo alifunga mabao mawili Real Madrid ilipoilaza Osasuna kwenye fainali ya Copa del Rey mjini Seville na kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza tangu 2014.

Real Madrid, ambao ndio kwanza wameshinda ubingwa wao wa ishirini wa Copa del Rey, sasa wataangazia mechi yao ya nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City Jumanne.

Ndani ya sekunde 106 tu baada ya mchezo kuanza, Rodrygo aliifungia Real bao la kwanza na likawa bao la haraka zaidi kuwahi kufungwa katika fainali ya kombe la Uhispania katika miaka 17. Rodrigo pia katika dakika ya sabini alitikisa nyavu na kuoneza bao la pili ambalo lilipelekea Real Madrid kutwaa kombe hilo.

Carlo Ancelotti, kocha mkuu wa Real Madrid, alisema kwamba timu yake "itacheza na wachezaji 12 dhidi ya 11," katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City Jumanne.

Copa del Rey - Final - Real Madrid v Osasuna

Ancelotti alisisitiza umuhimu wa wafuasi wa klabu hiyo kwa matarajio yao ya mafanikio. Vilabu hivyo viwili vitamenyana Bernabeu kwa mkondo wa ufunguzi wa mechi yao ya nne bora barani ulaya.

Copa del Rey - Finali- Real Madrid  dhidi Osasuna

Mechi nane za awali za Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Man City zimeishia kwa ushindi mara tatu, kupoteza mara tatu na kutoka sare mara mbili kwa Real Madrid.

Copa del Rey - Final - Real Madrid v Osasuna

"Tunajua kama leo na kama siku zingine huko Bernabeu, watatusukuma. Tuna faida ndogo katika mechi ya kwanza na hiyo ni kwamba tunacheza na wachezaji 12 dhidi ya 11, wafuasi wetu wakiwa ndio mchezaji wa kumi na mbili’’ alisema Ancheloti

TRT Afrika