Shirikisho la soka Afrika CAF limetoa droo ya mechi za ligi ya mabingwa ya wanawake 2023, huku vilabu nane vimewania ubingwa Cote D'ivoire kuanzia Novemba 5 hadi 19.

Sasa ni rasmi kuwa kila timu iliyofuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya wanawake ya Caf, Ivory Coast 2023 imemfahamu mpinzani wake na kujiandaa kwa ngarambe hizo zijazo.

JKT Queens ya Tanzania ambayo ni mwakilishi wa pili wa Tanzania katika fainali hizo ikifuata nyayo za kina dada wa klabu ya Simba Queens walioshiriki msimu uliopita, iliifunga CBE FC ya Ethiopia kupitia penalti kwenye fainali na kufuzu kwa mara yake ya kwanza.

CAF imefanya droo hiyo rasmi siku ya jumatatu, Oktoba 09 katika sherehe ya kufana iliyohudhuriwa na wawakilishi kutoka kanda sita za CAF, vilabu vinavyoshiriki pamoja na wadau muhimu wa soka barani afrika.

Droo hiyo ilifanywa na nguli wawili wa soka barani Afrika, wakiwemo Fernande Tchetche Wa Cote D'ivoire, pamoja na nahodha mshindi wa totalenergies WAFCON 2022, Janine Van Wyk wa Afrika Kusini

Mahasimu wa Jkt Queens ya Tanzania kundi A?

Timu ya wanawake ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini

  • Ni washindi wa kombe la kwanza la vilabu bingwa vya wanawake Afrika mwaka 2021 walipoifunga Hasaacas Ladies wa Ghana katika fainali iliyofanyika nchini Misri.
  • Ndio mabingwa mara nne wa mataji manne ya mwisho ya ligi kuu ya wanawake Afrika Kusini.

Timu ya wanawake ya Athletico FC d’ Abidjan kutoka Cote D'ivoire

  • Ndio mabingwa wa Cote D'ivoire 2022-23
  • Wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza kwa kuwa timu ya kwanza kutoka Cote d' Ivoire kufuzu kwa kombe la vilabu bingwa vya wanawake Afrika.

Timu ya wanawake ya SC Casablanca kutoka Morocco

Timu hiyo kutoka Casablanca iliundwa tu mnamo 2019 na imetinga fainali hizo kwa mara yao ya kwanza na kuwa mwakilishi wa pili wa Morocco katika fainali, baada AS FAR.

KUNDI A:

  • Athletico FC d’Abidjan (Cote D'ivoire)
  • Sporting Casablanca (Morocco) Mamelodi Sundowns
  • Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
  • JKT Queens (Tanzania)

KUNDI B:

  • AS FAR (Morocco)
  • Ampem Darkoa (Ghana)
  • Huracanes FC (Equatorial Guinea)
  • AS Mande (Mali)

Mashindano hayo yatafanyika katika miji miwili mizuri ya Cote D'ivoire ya San Pedro ugani (Stade Laurent pokou) na Korhogo katika uwanja wa (Stade Amadou gon Coulibaly) kati ya tarehe 05 – 19 November mwaka huu.

TRT Afrika