Ushindi wa Arsenal Jumapili itaiweka pointi mbili nyuma ya Liverpool, ambao ndio viongozi wa ligi na pia kurudi katika nafasi ya pili ikisubiri matoeko ya mechi kati ya Manchester City na Brentford Jumatatu usiku.
Hata hivyo, vijana wa Klopp wanaongoza kileleni kwa pointi tano huku Manchester City ikiwa ya pili nayo Arsenal ikiwa katika nafasi ya tatu.
Mchuano wa kukata na shoka kati ya Arsenal na Liverpool hata hivyo umegubikwa na majeraha kwa baadhi ya wachezaji wa pande zote mbili.
Liverpool huduma za Mohamed Salah, Joel Matip, Kostas Tsimikas, Stefan Bajcetic na Ben Doak wanaouguza majeraha.
Wakati huo huo, mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay, Darwin Nunez anadaiwa kuwa na tatizo la mguu ambalo linaweza kumzuia kuingia uwanjani jumapili dhidi ya Arsenal.
Nunez aliondoka Anfield akivaa buti ya kutembea baada ya kujeruhiwa mapema kwenye ushindi wa 4-1 wa Liverpool dhidi ya Chelsea katikati ya wiki, meneja Jurgen Klopp alisema Ijumaa.
"Tunazingatia tu mchezo, juu ya mambo tunayopaswa kufanya, kujiboresha kutoka michezo tuliyocheza dhidi yao na kujifunza kutoka kwa michezo tuliyocheza dhidi yao kwa sababu ni wazuri sana, na kujaribu kushinda," Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema.
Arsenal itakuwa bila kiungo Thomas Partey kwenye kipute dhidi ya Liverpool kufuatia maumivu zaidi kwenye jeraha lake.
Tomiyasu, na Endo wamekuwa katika Kombe la bara Asia wakiiwakilisha Japan na hawatokuwa mechi hiyo.