Ifikapo siku mwisho ya hatua ya mchujo wiki hii, mataifa yote 24 ya Afrika yaliyofuzu kwa tamasha kubwa la soka barani yatathibitishwa rasmi.
Awali, Cote d'Ivoire (wenyeji), Morocco, Algeria, Afrika Kusini , Senegal, Burkina Faso, Tunisia, Misri, Zambia, Equatorial Guinea, Nigeria, Cape Verde, Guinea Bissau, Mali, na Guinea zilijikatika tiketi za kushiriki kwenye michuao ya CAF huko Abidjan mwakani.
Angola imejiunga na Tanzania na Ghana na kujihakikishia tiketi ya kurejea katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies 2023 baada ya kutoka sare ya 0-0 na Madagascar katika mchezo mwingine wa kundi E.
Ratiba kamili ya mechi za siku ya Jumamosi.
- 9-Sep-2023 Malawi VS Guinea 13h00 Group D
- 9-Sep-2023 Comoros VS Zambia 19h00 Group H
- 9-Sep-2023 Cote d'Ivoire VS Lesotho 16h00 Group H
- 9-Sep-2023 Mauritania VS Gabon 16h00 Group I
- 9-Sep-2023 Congo DR VS Sudan 16h00 Group I
- 9-Sep-2023 Morocco VS Liberia 19h00 Group K
- 9-Sep-2023 Mozambique VS Benin 13h00 Group L
- 9-Sep-2023 Senegal VS Rwanda 19h00 Group L
Makala ya 34 ya shindano hilo la soka linalotazamwa zaidi Afrika, yataanza nchini Cote d'Ivoire kati ya Januari 13 na 11 Februari huku ikichezwa na mataifa 24 yenye nguvu barani Afrika katika kile kinachoahidiwa kuwa toleo lenye ushindani mkali la TotalEnergies CAF, Kombe la Mataifa ya Afrika.
TRT Afrika