Walid Regragui alipigwa marufuku kwa mechi nne. Picha: Nyingine

Kocha wa Morocco Walid Regragui alifanikiwa kuondolewa marufuku kwa mechi mbili katika Fainali za Mataifa ya Afrika siku ya Ijumaa, na kumpa kibali cha kuchukua usimamizi wa mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Afrika Kusini.

Regragui, ambaye aliipeleka Morocco katika nusu-fainali ya Kombe la Dunia mwaka wa 2022, alisimamishwa kufuatia kuzozana na nahodha wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Chancel Mbemba wakati wa mchezo wa kundi.

"Kughairiwa huku kunahusu pia faini iliyotolewa na mahakama ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Bw. Regragui," ilisema taarifa ya Shirikisho la Soka la Kifalme la Morocco (FRMF).

Mchuano wa hatua ya 16

"Maamuzi ya mahakama ya rufaa yanakuja kufuatia hoja za utetezi zilizowasilishwa na FRMF."

Regragui alipigwa marufuku kwa mechi nne lakini mbili zikasamehewa.

Alitumikia mechi moja ya marufuku yake dhidi ya Zambia siku ya Jumatano na nafasi yake ikachukuliwa na msaidizi wake Rachid Benmahmoud.

Morocco itakutana na Afrika Kusini katika hatua ya 16 bora Jumanne ijayo mjini San Pedro.

TRT Afrika