Wizkid playing at Tottenham

Na Kudra Maliro

Ayodeji Ibrahim Balogun, almaarufu Wizkid aliingia kwa kishindo wakati wa tamasha lake kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur jijini London. Hili itasalia kukumbukwa na wapenzi wa muziki wa Kiafrika

Wizkid alifanya onyesho la ajabu wakati wa tamasha lake la "More Love Less Ego" kwenye uwanja wa Spurs jijini London Jumamosi tarehe 29 Julai 2023, na mashabiki wake na wapenzi wa burudani walishindwa kujizuia.

Tamasha la London ni tukio muhimu kwa muziki wa Kiafrika, kwani mwimbaji huyo ndiye msanii pekee wa Kiafrika aliyeandaa na kujaza mashabiki kwenye uwanja huo.

Akiingia kwa madaha na wimbo wake wa Reckless, uliotolewa kutoka kwa albamu iliyoshinda Tuzo ya Grammy, Made in Lagos, umati haukuweza kuficha furaha yao alipopanda jukwaani.

Juhudi za ushirikiano

Kama ilivyotarajiwa, nyota huyo wa Nigeria, mmoja wa wanamuziki mashuhuri zaidi wa Kiafrika, alitoa mchanganyiko uliotiririka wa R&B, hip-hop na Afrobeat, na kushangiliwa na umati wa watu kutoka matabaka mbali mbali.

Tamasha limetoa maoni tofauti. Picha : Tottenham Hotspot Stadium/Twitter

Maoni kuhusu tamasha hili la kihistoria yalichanganywa, huku mashabiki wa nyota wengine kama Davido na Burnaboy wakisema kuwa hadhira haikujaa kama ilivyotarajiwa.

Tukio hilo lilizua mjadala. Baadhi walihoji ukweli wa ripoti kwamba tamasha hilo lilikuwa limejaza mashabiki na karibu tikiti 60,000 ziliuzwa.

Kwa vyovyote vile, ukubwa wa tukio hilo na miitikio ya wale walioshiriki huonyesha mafanikio yake.

Wizkid ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, amefanya kolabo na wasanii maarufu duniani kama vile Drake, Chris Brown na Justin Bieber. Uchezaji wake huko London uliimarisha nafasi yake kama mmoja wa watu maarufu wa Afropop.

Utandawazi wa muziki wa kiafrika

Tamasha hilo lilishirikisha wageni maalum Masego na Cavemen. Masego, anayejulikana kwa mchanganyiko wake wa R&B, hip-hop, funk na Afrobeat, pia aliwarusha roho mashabiki.

Kifedha, tamasha hilo lilikuwa la mafanikio makubwa kwa Wizkid. Kulingana na makadirio ya juu juu , mauzo ya tikiti yalileta kati ya £3.6 na £4.8 milioni, kulingana na tikiti 60,000 zilizouzwa. Takwimu hizi zinasisitiza uwezo mkubwa wa kifedha wa aina hii ya tukio.

Tamasha hilo lilivutia hisia kutoka kwa mashabiki na watu mashuhuri, huku wengi wakionyesha kuvutiwa na mchango wa Wizkid katika utandawazi wa muziki wa Kiafrika.

Zaidi ya onyesho la muziki, hafla hiyo ilikuwa sherehe ya utamaduni wa Kiafrika, talanta na ushawishi wa kimataifa wa Afrobeat.

TRT Afrika