Feven & Helena Yohannes
Baba yetu alikuwa mwanamapinduzi. Akiwa mpiganiaji wa uhuru na kiongozi katika vita vya Eritrea na Ethiopia.
Jicho lake la kushoto lilikuwa kipofu baada ya kupigwa na mlipuko wa bomu la ardhini, alilazimika kutoka katika nchi yake ya kuzaliwa kwasababu alikuwa akikashifu uongozi ambao haukuwa wa kidemokrasi.
Hadithi yetu ilianza kabla ya kuzaliwa, wakati baba yetu akiwa nusu kipofu na mama mjamzito walipotembea kutoka Asmara nchini Eritrea hadi kambi ya wakimbizi huko Gibra nchini Sudan - sawa na kutembea kutoka Los Angeles hadi San Francisco Marekani .
"Ilituchukua miezi michache," baba yangu alituambia wakati mmoja akiwa na tabasamu usoni, "lakini tulifika huko."
Walifanya hivyo kwani hawakuwa na chaguo. Hawakuwa na pesa, wakiwa wamevaa nguo tu walizokuwa nazo.
Mama yetu alituzaa kwenye kibanda kilichojengwa kwa udongo na nyasi, huku baba yetu akiwa amesimama nje akisubiri kilichotokea kuwa mshtuko wa maisha yake.
Kwa kuwa hawakuwa na teknolojia ya kuwafahamisha mapema kuhusu jinsia ya mtoto wao, waliamini kuwa walikuwa na mvulana mdogo kwa kuwa mama yetu alikuwa na urefu wa futi tano tu na uvimbe wake wa mtoto ulionekana kuwa mkubwa isivyo kawaida. Lakini hapana, walitupata sisi, watoto wa kike mapacha wanaofanana!
Wazazi wetu walijua kambi ya wakimbizi walipokuwa haikuwa mahali pa kulea familia. Maskini, bila chochote ila imani tu, mama yangu alituma ombi kwa mpango wa uhamisho wa wakimbizi wa Marekani. Ilichukua mwaka , lakini kupitia imani yake na kuendelea kwake, tulichaguliwa.
Ilimaanisha kwamba tungelazimika kuacha familia yetu kubwa, kuacha kila kitu tulichokuwa tumewahi jua, kwa ajili ya makaazi mapya huko Rochester, jijini New York, Marekani—mahali ambapo pangetulea na kutuunda milele .
Tulipofika Marekani, tulilazimika kujifunza lugha mpya kuzoea maisha na utamaduni tofauti kabisa.
Miaka yetu michache ya kwanza huko Marekani ilikuwa ngumu.
Wazazi wetu walijitahidi kadiri wawezavyo kutukinga na uwoga. Walitulea , watoto wanne bila uwezo mkubwa wa kifedha, katika nchi wasiyoijua.
Baba yetu alifanya kazi kama mlinzi, na mama yetu kama mlinzi wa nyumba ya kanisa ambayo ilitufadhili. Wakikazana hivyo pamoja na kuenda katika madarasa ya kujifunza kingereza kipaumbele chao kikuu kilikuwa kututunza.
Licha ya changamoto hizo nyingi, hawakukata tamaa katika ndoto zao. Iliwachukua miaka mingi , lakini hatimaye baba yetu alipata shahada ya uzamili katika usimamizi wa umma na mama yetu akaanza kazi ya uuguzi.
Kushuhudia njia ndefu na ngumu ya wazazi wetu kutoka kwa mapambano hadi ushindi - bidii yao na uvumilivu, matumaini yao yasiyotikisika na uwezo wa kukumbatia changamoto kama fursa za kukua - vilitufanya tulivyo kuwa, na sisi ni nani.
Tumezoea kuwa wavumilivu na watulivi kwa maisha. Ukakamavu wa kiakili, na imani - tabia za wazazi wetu - zilituunganisha tulipokuwa tukikua, tukachukua hatua kubwa ya kuhama kutoka kwa wazazi wetu wapendwa, kutoka Rochester hadi Los Angeles, na kuwa wajasiriamali.
Sasa tunahusika na biashara ,Feven ni mtaalamu wa mapambo ya ndani , na Helena ni mtaalamu kwa biashara ya matangazo.
Mbali na hii pamoja tuliunda biashara ya urembo inayoitwa 2•4•1.
Tulibuni jina hili 2.4.1 kwa kimobo Two four one – kutokana na watu wengi kutuagalia na kututania wakituuliza kama tulikuwa watu waili kwa mmoja .
Wengine walikuwa wakiuliza kati yetu ni nani pacha mwenye nidhamu zaidi .
Biashara hii ya 2•4•1 brand ni onyesho la imani yetu kwamba wanawake ni akili na uzuri pia - hatuna budi kuchagua moja au nyingine; tunaweza kuwa wote wawili. Tukiwa njiani kutoka sehemu ya mashariki ya Afrika hadi ufuo wa magharibi wa Amerika
Muda mfupi baada ya kuanza 2•4•1, kama wamiliki wa biashara tuliona moja kwa moja jinsi janga la COVID -19 lilivyokuwa likiharibu mauzo yetu wenyewe na uchumi kwa ujumla, na tulikuwa na wasiwasi kuhusu kuendelea kwa kampuni yetu. Lakini kupitia mitandao ya kijamii, tuliweza kuungana na kujifunza zaidi kuhusu wateja na wafuasi wetu.
Ndani ya nyumba zetu huko Los Angeles (ambazo zimetengana kwa umbali wa mita tatu tu), kila mmoja wetu ana picha mbili kwenye dawati yake.
Ya kwanza ni yetu tukiwa wasichana wadogo, ukumbusho wa kila siku wa kutokuwa na hatia na udadisi wetu.
Ya pili ni picha ya Oprah Winfrey akiwa ameshikilia bidhaa ya 2•4•1 ya vipodozi. Ni uwakilishi wa kuona kuwa ndoto yetu imetimia.
Kutambuliwa na mtu anaye ushawishi na anayeheshimiwa kama Oprah, mtu aliyebadilisha ulimwengu, kumeathiri biashara yetu kwa njia ambazo bado hatujaamini.
Alipokutana na bidhaa zetu za 2.4.1 na kuzikubali Oprah hakujua kuwa ni kitabu chake, “What I Know for Sure,” ambacho kilikuwa kimetupa imani na nguvu ya kuendekea kujijenga .
Hakujua kwamba sauti yake na masomo aliyotufundisha kupitia kitabu hicho kilikuwa tayari kimetumika kama nyota yetu ya Kaskazini katika safari yetu ya ujasiriamali.