Rotavirus: Unachopaswa kujua kuhusu mlipuko wa virusi vya Rota Kenya

Rotavirus: Unachopaswa kujua kuhusu mlipuko wa virusi vya Rota Kenya

Mombasa inasema kesi tatu za virusi vya rota zimethibitishwa
Mombasa, Pwani ya Kenya inaweka mikakati ya kumaliza maambukizi ya virusi vya rota./ Photo: AFP

Kaunti ya pwani ya Kenya, Mombasa imeanza zoezi la jumla la chanjo kwa watoto dhidi ya virusi vya rota. Virusi vya rota vinasababisha kuhara na inaathiri sana watoto wachanga na watoto wadogo.

"Kwa sasa tuna dozi za kutosha za chanjo , idara ya afya ya umma itashirikisha mara moja wafanyakazi wa jamii, na watu wa kujitolea," gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir amesema.

“Maradhi haya yanatokea hata kama maji ni masafi , ukiwa umeshika choo na haukunawa kisha sasa ukatia kitu ndani ya mdomo , haihusiani na mambo ya mvua,” ameongezea.

Maambukizi ni rahisi kwa watoto wenye umri wa miezi 3 hadi 35. Kaunti hiyo imesema ugonjwa huo umezuka kutoka kwa kituo cha kulelea watoto mchana katika eneo liitwalo Shomoroni eneo la Kisauni.

Halamashauri ya kaunti imetishia kufunga maeneo yoyote ya mafunzo au yakutunza watoto yatakayopatikana kuwa hayafikii viwango kinavchoitajika cha usafi.

Je tunafaa kujua nini kuhusi virusi vya Rota?

• Virusi vinaweza kusababisha kuharisha sana, kutapika, homa, na maumivu ya tumbo

• Watoto wanaombukizwa na virusi vya rota wanaweza kukosa maji mwilini na kuhitaji kulazwa hospitalini

• Watu wazima wanaogusana au kuhusiana kwa ukaribu na watoto wadogo walioambukizwa na virusi vya rota wako katika hatari ya kuambukizwa pia

• Kuna chanjo aina mbili dhidi ya virusi vya rota vilivyoidhinishwa na shirika la Afya duniani Rotarix na Rotateq

• Mtu aliyeambukizwa na virusi vya rota anaweza kuisambaza kwa kugusa kitu chochote, ikiwa ni pamoja na chakula, midoli na vyombo

• Ili kuzuia maambukizi watu wanashauriwa kunawa mikono vizuri na mara kwa mara, Ni muhimu pia kuzingatia usafi kwa mambo mengine kama upishi, mauzo ya chakula sokoni , mahotelini na maeneo mengine

• Chanjo dhidi ya virusi vya rota ilianzishwa katika mpango wa kawaida wa chanjo ya watoto wachanga nchini Kenya mnamo Julai 2014

TRT Afrika