Sauti Sol

na

Charles Mgbolu

Mashabiki wa bendi na kundi la Afropop la Kenya lijulikanalo kama Sauti Sol wanajiandaa kusema kwaheri ambayo itakumbana na vilio ikiwa ni siku ya mwisho ya tamasha na onyesho la bendi hiyo ambapo watatumia nafasi hiyo kuaga kwa Mashabiki na kuvunja rasmi kundi hilo lenye jina katika bara la Afrika na duniani kote.

Sauti Sol ilitoa tangazo la kushtua mnamo Mei 2023 kwamba kikundi kilikuwa kinafanya matamasha ya mwisho kikielekea kusambaratika baada ya miaka 18 pamoja na washiriki mmoja mmoja wangesitasita kwa muda usiojulikana baada ya kumalizika kwa tamasha la mwisho la kuaga lililopangwa kufanyika Novemba 2 jijini Nairobi.

Hata hivyo, tiketi za tamasha zimekuwa zikiibua gumzo mtandaoni na nje ya mtandao, huku mashabiki wengi wakichukua mara mbili kwa bei iliyoambatanishwa nazo.

Hafla hiyo yenye hadhi ya VIP itagharimu mashabiki shilingi 20,000 za Kenya sawa na Dola za Kimarekani 138 ($138), kulingana na waandaaji.

Tamasha hilo linajumuisha chakula cha jioni, vinywaji, kifurushi cha bidhaa cha Sauti Sol, na kukutana na kusalimiana na Sauti Sol, na zaidi ya yote, onyesho la jukwaani la Sauti Sol.

Bendi hiyo imeahidi kutumbuiza na kungonga mioyo ya mashabiki wao, ikisema, ‘’Sio mwisho wa enzi tu, bali ni mwanzo wa urithi ambao utabakia kukita mizizi katika mioyo ya mashabiki wao.’’

Lakini bei ya tiketi inawaondoa mashabiki wengi wa nyota hao kwenye tafrija yao kutokana na gharama yake.

‘’Nyinyi hamwezi kutufanyia hivi, aliandika @terrylnemboya kwenye X, zamani Twitter.

‘’Itanibidi kuchungulia ili kutazama tamasha, aliandika shabiki mwingine, @reccro, pia kwenye X.

Wengine walikikumbusha kikundi hicho kuhusu gharama kubwa ya maisha inayopatikana kwa sasa nchini Kenya, huku wengine wachache wakiuliza ikiwa kikundi hicho kilipanga kufanya kisichowezekana wakati wa hafla hiyo.

Licha ya ukosoaji huo, mashabiki wengi wamejitokeza kuwatetea akiwemo mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Kenya Bensoul. ‘’Ikiwa ni vigumu kwako kuongeza 20,000 kufikia Novemba, basi una safari ndefu. Wacha sisi ambao ni matajiri tuende kwenye tamasha kwa sababu burudani itakuwepo,'' aliandika kwenye X.

Sauti Sol

Tweet yake iliibua mtafaruku zaidi kutoka kwa mashabiki, na kuwalazimu bendi hiyo ya Sauti Sol, Bien Aime Baraza na Savara Mudigi kuzungumza hadharani kuhusu suala hilo.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya ndani, walisisitiza kuwa bei za tiketi ni halali.

"Tunakupa miaka 20 ya maisha yetu; tumekuwa pamoja kwa miaka 20. Bei hiyo ya tiketi ina thamani ya miaka 20 ambayo tumekuwa pamoja," Bien alisema.

Savara aliongeza kuwa bei za tiketi pia zinaonyesha kupanda kwa gharama ya maisha na gharama kubwa za uzalishaji wa tamasha hilo.

"Gharama ya kufanya tamasha ni ghali pia. Hatujaribu kuchukua faida ya watu," Savara alisema.

Bendi hiyo pia ilisema wanataka kuwapa mashabiki wao uzoefu wa kukumbukwa kwenye tamasha hilo.

Polycarp Otieno and Savara Delvin Mudigi wa Sauti Sol, wakati wa tamasha la Sol Fest Concert mjini Nairobi, Kenya

Mjadala bado unaendelea huku bei ya tiketi ikiwa imewafanya mashabiki kugawanyika sana, huku mashabiki wakali wakiapa kupambana na maisha na hali ya uchumi ili kununua tiketi hizo.

Wadadisi wa muziki, hata hivyo, wana imani kwamba tamasha la mwisho litafana na tiketi zote zitauzwa , na tiketi zisizo za VIP ambazo zimegharimu shilingi 2,500 za Kenya tayari zimeuzwa kwa muda wa mwezi mmoja tu baada ya kuingia kwenye viwanja vya tiketi.

TRT Afrika