Virusi ya Marburg, jina lake kutoka mji wa Ujerumani, ambapo ulitambulika kwa mara ya kwanza mnamo 1967. Visa vya hivi punde vimeripotiwa nchini Tanzania na Equatorial Guinea.
Marburg (MVD) ni homa hatari ya kuvuja damu isiyo na chanjo au tiba inayojulikana na imeweka ulimwengu kwenye tahadhari ya afya na wanasayansi walikuwa wakiharakisha kutafuta chanjo.
Shirika la Afya Duniani siku ya almamis wiki iliyopita lilitangaza visa 8 vya ugonjwa huo huko Equatorial Guinea.
Kesi hizo mpya zilithibitishwa baada ya sampuli ya maabara kuchunguzwa "Kie Ntem mashariki, Litoral magharibi mwa nchi hiyo, na mkoa wa Centro Sur, unaopakana na Cameroon na Gabon," WHO ilisema.
Maeneo yanaoripoti kesi ni kama yamepishana kama kilomita 150 (maili 93), ishara ya kuenea kwa virusi hivyo, ilisema WHO.
Angalau kesi 20 zimeripotiwa na vifo 20.
Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, alisema uthibitisho wa kesi hizo mpya ni ishara muhimu ya kuongeza juhudi za kukabiliana na kukomesha haraka mlolongo wa maambukizi na kuepusha uwezekano wa milipuko kubwa na vifo.
Unapaswa kufahamu nini kuhusu ugonjwa wa Marburg?
Marburg, ni kirusi kinachoambukiza na ni hatari sana, vinahusiana na binamu yake - Ebola. Hizi ni sehemu ya kundi pana la virusi vinavyoweza kusababisha homa ya virusi ya kuvuja damu, dalili ya homa na kutokwa na damu.
Virusi ya Marburg ilichukua jina lake kutoka mji wa Ujerumani, ambapo iligundulika kwa mara ya kwanza mnamo 1967 kufuatia kuingizwa kwa nyani wa Kiafrika kutoka Uganda, ambao baadaye waliambukiza wafanyakazi wa maabara huko Ujerumani na Yugoslavia.
Milipuko imetokea katika nchi chache ya Afrika, tangu wakati huo, lakini mara chache zaidi kuliko Ebola. Kubwa zaidi lilikuwa nchini Angola mnamo 2005, na kesi 374 na vifo 329.
Janga kubwa la Marburg limetokea Angola mwaka 2005 ambapo watu 329 walifariki.
Hata hivyo, hivi karibuni nchi ambazo zimeripoti virusi vya Marburg ni pamoja na Ghana, Guinea, Uganda, Kenya, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Urusi, Zimbabwe, Afrika Kusini, Yugoslavia na Ujerumani, na kuibua wasiwasi juu ya uwezekano wa virusi hivyo kuwa kubwa, tena janga kubwa yenye uwezo wakuenea duniani kote kama Uviko-19.
Maambukizi na dalili
Virusi huenea kati ya watu kupitia kugusa majimaji yatokayo kwa mgonjwa mwenye dalili, haswa kwa maji ya mwili, kama vile damu, matapishi na kinyesi. Inaweza pia kuambukizwa kwa kujichanganya na wanyama walioambukizwa, kama vile popo au nyani.
Kulingana na maelezo ya WHO, virusi vya Marburg vinaweza kusababisha homa kali ya hemorrhagic, na kusababisha kushindwa kwa shinikizo na kifo.
Kiwango cha vifo vya virusi hivyo kinakadiriwa kuwa kati ya asilimia 24 na 88, kulingana na mlipuko huo.
Ingawa utambuzi wa kimatibabu wa MVD ni mgumu, virusi vya Marburg na virusi vya Ebola ni washiriki wa familia moja, inayojulikana kama Filoviridae, na wana dalili sawa na njia za maambukizi.
Dalili za virusi vya Marburg zinaweza onekana ndani ya siku 2-21 baada ya kuambukizwa.
Dalili za virusi huonekana kwa mtu aliyeathiriwa kama homa kali. Hali hii huambatana na maumivu ya kichwa, kutapika damu, maumivu ya viungo na misuli na kutokwa na damu bila maelezo kupitia matundu ya mwili, yakiwemo macho, pua, fizi, masikio na ngozi.
Tunapaswa kuwa na hofu?
Mlipuko wa virusi vya Marburg nchini Guinea umeibua wasiwasi kutokana na ukaribu wa nchi hiyo na mataifa mengine ambayo yamekumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola siku za nyuma zikiwemo Sierra Leone na Liberia.
Wasiwasi ni kwamba Marburg inaweza kuenea kama Ebola ya mwaka 2014, kusambaa na kuwa mlipuko mkubwa zaidi wa kimataifa. Inaweza kuenea kwa mataifa mengine mengi kutokana na safari za watu mbalimbali. Mwaka 2014 tulishuhudia ongezeko la visa vya Ebola kutoka Guinea hadi Liberia na Sierra Leone.
Kesi nyingi zilitokea katika mataifa haya matatu, hata hivyo kesi zilizounganishwa na watu kusafiri pia zilitokea katika mataifa mengine saba, pamoja na Marekani na Uingereza.
Kwa mfano huo ugonjwa uliweza athiri usafiri kwenda Uingereza na Marekani.
Licha ya utafiti tofauti juu ya wanyama, hakuna matibabu maalum au chanjo ya ugonjwa wa virusi vya Marburg. Matibabu ya majaribio hayajawahi kujaribiwa kwa wanadamu.
Afrika CDC wanaeleza kwamba itifaki zilizopo za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya Ebola na homa nyingine za virusi za kuvuja damu zinaweza kutumika kuzuia maambukizi ya MVD.
WHO imesema inashirikiana na mamlaka za kimataifa kuongeza hatua za kukabiliana na dharura - ikiwa ni pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa, upimaji, huduma za matibabu, kuzuia na kudhibiti maambukizi pamoja na kufanya uchunguzi zaidi wa magonjwa.
Ikisisitiza haja ya kuongeza ufahamu wa wananchi ili kusaidia kuzuia kuenea kwa maambukizi, WHO ilisema wataalam wa ziada wa magonjwa ya mlipuko na kuzuia na kudhibiti maambukizi watatumwa katika siku zijazo.
Afrika CDC kimesema kitatuma timu ya wataalamu nchini Tanzania kusaidia katika hatua za kukabiliana na ugonjwa huo.