Shayiene and her team at the 2022 International Blackball Championship in Morocco. ionship in Morocco.

Msichana huyo wa Afrika Kusini ambaye maisha yake amekulia katikati ya mitaa yenye vurugu na magenge ya vijana waliogubikwa na tabia mbaya na za kihuni alifanikiwa kupambana na kuyashinda maisha hayo ya utotoni na kuibuka bingwa wa dunia katika mchezo huo ambao anasema "uliokoa maisha yake"

Shaiyene Fritz, 22, anazungumza kuhusu safari yake ya utotoni kutoka kwenye maisha ya giza ya maeneo ya Lavender Hill ya Cape Town mtaa uliojaa majambazi kwa vipindi vyote vya siku kuanzia Asubuhi kwenye mwanga hadi Jioni kwenye giza. Mtaa huo umezidi kuwa maarufu kutokana na makundi hayo ya kihalifu na uhalifu huo umechochewa na kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Afrika Kusini imekuwa maarufu kwenye kupata mataji ya bingwa wa pool na hiyo imedhihirika kwa Shaiyene baada ya kujinyakulia medali zikiwemo medali tano za dhahabu na tatu za fedha.

"Unapokuwa mtoto huko Lavender Hill, unakabiliwa na vitu vingi sana hivi kwamba unalazimika kukua kufuatana na mwenendo wa mitaa hiyo na ni nadra na Huwezi kufurahia utoto wako kama watoto mahali pengine," anaiambia TRT Afrika.

Ligi Ndogo

"Eneo hilo ni kitovu cha majambazi, na kuna kiwango kikubwa cha mimba za utotoni. Kuishi katika eneo ambalo unakabiliwa na haya yote, ni vigumu kustawi na kufanikiwa" anaongeza.

Shayenne alianza kucheza pool akiwa na umri wa miaka tisa. Picha: Shayenne

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch anakumbuka kwamba akiwa na umri wa miaka tisa tukio la kupoteza kazi kwa mamake kulilazimisha familia kuhama kutoka nyumba ya vyumba vitatu hadi kwenye kibanda cha chumba kimoja huko Lavender Hill.

Mbaya zaidi tukio lingine lilofuata ni lile la Majambazi walimdunga kisu kaka mkubwa wa Shaiyene mnamo mwaka 2018, na kumwacha hospitalini kwa mwezi mmoja.

"Ndugu yangu aligombana na mtu aliyehusishwa na genge moja la eneo hilo. Majambazi hawa walitaka kumuua kwa ajili yake," anasema. "Unapokua katika eneo hili unajaribu kujiepusha na majambazi kadri uwezavyo. Lakini wakati mwingine inakupata tu. Magenge mbalimbali yanakuja kukutafuta."

Akiwa mwanafunzi wa darasa la 9, Shaiyene alilazimika kufyatua risasi alipokuwa akirejea nyumbani kutoka shuleni siku moja.

Jumuiya ya wanafunzi ilimuunga mkono Shaiyene na $2,000 ili kuhudhuria mashindano nchini China mwaka huu. Picha: Shaiyene

"Ghafla kulitokea kurushiana risasi, ikabidi tukimbilie kwenye nyumba ya jirani ili kujificha hadi milio ya risasi ikaisha. Unapokua Lavender Hill, unakuwa umezoea mambo kama haya. Unasikia risasi mara kwa mara, hata huku wewe ukiwa umelala kitandani kwako, na risasi zinafyatuliwa karibu na nyumba. Watu wameshazoea hali hiyo na wameshachukulia kawaida kuonekana kwa matukio hayo " anasema.

Katika safari yake hiyo Bingwa huyo kwenye mazingira ya vurugu, Shaiyene alitafuta hifadhi katika maduka ya michezo ya Lavender Hill ambayo yalijumuisha meza za michezo ya pool na sehemu za kuogelea. Alitumia muda wake mwingi wa mapumziko huko, ndipo baadae akapendezwa na michezo hiyo akiwa na umri wa miaka tisa na ndipo kipaji chake kilikuwa maradufu Bingwa huyo ilibidi atumie takribani randi 10 ili kuweza kucheza michezo hiyo na zilikuwa pesa zilizotumika vizuri.

Shayiene akiwa na washiriki wa timu yake Elzette Koen na Alexia Julius walishiriki katika shindano nchini Urusi. Picha: Shaiyene

"Kwanza tulianza kucheza dhidi ya maduka mengine katika eneo ambalo lilikuwa na michezo ya kuogelea na meza za pool. Tuliiita ligi ya kijamii, na mara nyingi nilifanikiwa kuwashinda wavulana," anasema Shaiyene.

Kadiri muda ulivyosonga, ujuzi wake ulizidi kuongezeka, na hatimaye akavuta hisia za waajiri wa michezo wenye ushindani. "Niliajiriwa kuchezea timu dhidi ya maduka mengine ya michezo ya ligi ya jamii. Tulifanya hivyo kwa takriban mwaka mmoja; kisha tukaanza kucheza ligi ya mkoa."

Mnamo 2015, Shaiyene na timu yake walishinda ubingwa wa kitaifa. Huu ulikuwa wakati muhimu kwake, na baadaye angeshinda kombe lingine wakati akiichezea timu ya wanawake.

"Mnamo 2016, tulitetea taji letu. Huu pia ni mwaka ambao nilichezea timu ya wanawake kwa mara ya kwanza. Nilikuwa mdogo katika timu, na tukaishia kushinda ubingwa wa wanawake wa 2018,"

Mchezo wa kijanja

Kucheza katika ngazi ya kitaifa tangu 2015 kumekuja na gharama mbalimbali ambapo Shaiyene wakati mwingine ilibidi kutafuta pesa zinazohitajika kuhudhuria mashindano.

"Nimechangisha hadi dola za Marekani 526 kwa mwaka kulipia angalau mashindano mawili. Nilikua na mama mmoja asiye na kazi, imetubidi kuja na pesa kwa namna fulani," anasema. "Nimezunguka vitongoji nikiuza tikiti. Nimekuwa nikichangisha fedha tangu 2014."

Kwa mchuano wake wa kwanza wa kimataifa nchini Urusi, Shaiyene alihitaji kuchangisha dola 160 - lengo ambalo alitimiza kwa urahisi. Lakini wakati mwingine amesafiri kwenda kwenye mashindano akiwa na chakula cha kutosha.

Mwaka jana, alisafiri kwa tiketi ya basi la njia moja kutoka Cape Town hadi Johannesburg kushiriki katika Mashindano ya Blackball ya Afrika Kusini. Akiwa na Dola 10 pekee mfukoni, hakujua jinsi angerudije nyumbani. Lakini safari hiyo ilizaa matunda aliposhika nafasi ya 9 katika kundi lake, na kufuzu kuwa sehemu ya timu ambayo ingewakilisha Afrika Kusini kwenye Mashindano ya Dunia nchini Morocco.

"Kila mmoja alipata takriban randi 500 kama pesa za zawadi, ambazo zilitosha kulipia tiketi za basi langu la kurudi nyumbani," Shaiyene anasimulia. "Kwa safari ya Morocco, ilinibidi kuchangisha takriban rand 40,000 (dola 2,100). Niliandaa Biashara ya soseji kwa usaidizi wa mpenzi wangu. Tuliuza roli kwa takriban $2 kila moja."

Lakini kuuza soseji haikutosha kupata pesa zinazohitajika. Mara tu baada ya muda, kampuni ya Afrika Kusini iliyobobea katika mchezo wa pool ilimpa Shaiyene nafasi ya ubalozi wa chapa hiyo.

“Nilitengeneza takriban randi 30,000, ambayo ni takriban dola 1500. Hiyo ilikuwa bahati sana kuwa mara yangu ya kwanza kupata kutambuliwa kutoka kwa kampuni kubwa. Ilinichukua miezi mitatu na nusu kupata pesa zote, na hiyo ilinipa nguvu niliyohitaji kufanya safari," anasema Shaiyene.

Mshindi wa Dunia

Ushindi mkubwa zaidi wa Shaiyene kufikia sasa ulikuja nchini Morocco, wakati yeye na timu yake waliposhinda taji la kimataifa. "Nilijivunia sana kwa kupata medali ya dhahabu. Ilikuwa furaha isiyo na kifani na ya kushangaza," anasema.

Mwanamke huyo mdogo anaishukuru familia yake na jumuiya ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch kwa kusaidia kazi yake kama mchezaji wa pool kitaaluma. Jumuiya ya wanafunzi ilichangisha dola 2,000 alizohitaji kuhudhuria mashindano mengine nchini China mnamo Machi mwaka huu.

"Walianza kuchangia na hata kuchapisha taarifa zangu kwenye mtandao wa TikTok, jambo ambalo lilisababisha michango zaidi kuja. Ghafla nilipata mchango mkubwa kutoka kwa mtu ambaye jina lake halikujulikana, ambaye alitoa rand 15,000, ambayo ni karibu $ 700," Shaiyene anasema. "Pamoja na hayo, nilipata pesa ambayo imetosha kununua tiketi yangu ya ndege kwenda China."

Aliporejea kutoka China, Shaiyene na mpenzi wake walianzisha Kituo cha kugusa maisha ya watu kiitwacho Shaiyene Fritz mwezi Mei. Taasisi hiyo inalenga katika kuwapa vijana fursa ya kupata elimu kupitia talanta, Karama na kufundisha vipaji.

“Kuna watoto wengi sana wanaohitaji kwenda Argentina kucheza soka, au England kucheza pia, lakini mama zao hawawezi kumudu,” anasema Shaiyene. "Ingekuwa vyema kuwaambia, 'Hapa kuna ufadhili kamili', ili wasipitie mapambano yaleyale niliyopitia kutafuta pesa."

TRT Afrika