Uamuzi wa Jeshi la polisi nchini Tanzania kuzuia maadamano ya leo yaliyoitwa na kundi la Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umetekelezwa vikamilifu.
Awali siku ya Jumapili, Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) uliitisha maandamano leo hii jumanne, tarehe 18 Julai, lakini licha ya hayo, hali ya utulivu imeshuhudiwa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini humo.
Akitoa wito kwa vijana nchini Tanzania, Mwenyekiti wa UVCCM Mohamed Ali Kawaida (MCC), alitangaza tarehe 18 kuwa siku ya maadaamano katika Wilaya zote na kuwaalika vijana ikiwa ni hatua ya kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari,
"Tunawahamasisha vijana wote wapenda maendeleo, vijana wote wanaopenda kuona serikali yetu na nchi yetu inaendelea, vijana wote wenye dhamira dhati na nchi yetu, tukutane Dar Es Salaam kwa maandamano rasmi ya kuunga mkono jambo la utekelezaji wa makubaliano haya. "
Polisi waliwashauri wanaolenga kufanya maandamano, kuwasilisha mawazo yao kupitia vyombo vya habari.