Mwimbaji maarufu wa kimataifa wa Nigeria Davido anaendelea kuvunja rekodi baada ya kuongoza chati ya Apple Music kama wimbo ulio sikilizwa zaidi katika siku ya kwanza ya kuachiwa kwake.
Rekodi hiyo mpya ilikuja saa 24 baada ya mwimbaji huyo kuweka rekodi mpya kwenye Spotify bila wimbo wowote kwenye albamu yake mpya, Timeless, kusikilizwa si chini ya mara 500,000 ndani ya siku ya kwanza ya kuachiliwa kwake.
Takriban nyimbo tatu zilisikilizwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya saa 48
Timeless pia imeweka rekodi mpya kwenye Apple Music, kwani sasa ndiyo albamu ya muziki iliyo sikilizwa zaidi na waafrika ndani ya saa 24 za kwanza baada ya kutolewa.
Kupitia ukurasa wao wa Twitter, Apple Music hawakuweza kujizuia kupongeza kazi mpya ya kimataifa ya Davido ambayo imebeba sura mpya ya soko la muziki wa Afrika kimataifa.