Waziri wa mazingira na malia asili nchini Kenya Aden Duale amesema kuwa serikali itaendeleza mpango wake wa kuwahamisha watu wanaoishi kando kando ya mito nchini.
Waziri Duale amesisitiza kuwa hii ni kwa maslahi ya wananchi kufuatia tishio la kutokea maafa kufuatia mafuriko ya mara kwa mara yanayosababisha kupasuka kingi za mito.
"Uhamishaji wa familia katika mito ya Nairobi ulikuwa wa halali, wa kibinadamu, na kwa manufaa ya wananchi kufuatia vifo vya watu kutokana na mafuriko jijini," alisema Duale.
Waziri huyo pia alisisitiza kuwa serikali itarejesha ardhi zote za umma katik amaeneo nyeti na yenye chimi chemi za maji.
Duale alikuwa akijibu masuali siku ya Jumanne mbele ya kamati maalum ya bunge juu ya mazingira, misitu na mali asili.
Hii inaambatana na agizo la mapema mwezi Mei ambapo serikali ilitoa makataa ya siku mbili kwa wote wanaoishi kando kando ya mito kuhama takriban mita 30 kutoka kingo za mito.
Mwezi huo taktiban watu 180,000 walihamishwa kutoka makazi yao.
Hata hivyo mwezi Mei, zaidi ya watu 47 walifariki katika mojawapo ya mafuriko mabaya kutokea nchini humo, na kile kinaonekana kuwa hali ya anga isiyotabirika kufuatia mabadiliko ya tabia nchi.