Waziri Agnes akitoka mahakamani

Waziri wa Uganda Agnes Nadutu ameachiliwa kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa tuhuma za kuiba mabati yaliyokusudiwa kwa wakazi wasiojiweza.

Waziri wa nchi anayehusika na masuala ya Karamoja alijisalimisha kwa polisi wiki tatu zilizopita na amekanusha mashtaka hayo.

Kesi yake itaanza baada ya wiki tatu na anakabiliwa na kifungo cha miaka saba jela iwapo atapatikana na hatia, vyombo vya habari vya nchini vinaripoti.

Nadutu ni waziri wa tatu anayekabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya vifaa vya ujenzi vilivyokusudiwa kwa mpango wa misaada katika eneo la kaskazini-mashariki la Karamoja. Wenzake pia wamekana kosa lolote.

Maafisa wengine wakuu serikalini pia wamehusishwa na kashfa hiyo. Rais Yoweri Museveni ametaka wale wote waliohusika kufunguliwa mashtaka.

Masharti ya dhamana ya Nadutu ni pamoja na kuweka hati yake ya kusafiria kwa mahakama.

Mkoa wa Karamoja ni eneo lenye ukame ambalo kwa miaka mingi limekuwa na ukame na mafuriko, huku watu wengi wakitegemea misaada.

TRT Afrika