Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wamefanya mazungumzo ya pamoja kuhusu hali ya maendeleo ya kikanda, vyanzo wa kidiplomasia vya Uturuki vimesema.
Katika mazungumzo ya simu siku ya Jumatatu, Fidan na Guterres walibadilishana mawazo kuhusu hali inayoendelea Gaza.
Tehran ilifanya mashambulizi zaidi ya 300 ya makombora na ndege zisizo na rubani kote Israel Jumamosi jioni katika kulipiza kisasi shambulio la anga la Tel Aviv kwenye ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria Damascus mnamo Aprili 1 ambapo wanachama saba wa Walinzi wa Mapinduzi wakiwemo majenerali wawili waliuawa.
Kuhusu maendeleo ya hivi karibuni Mashariki ya Kati, Uturuki ilisema itaendeleza juhudi za kuzuia kuzuka kwa mchakato ambao utaharibu kabisa uthabiti wa eneo hilo na kusababisha migogoro mikubwa zaidi duniani.
Ankara ilisema "kwa mara nyingine tena inatuma ujumbe wazi kwa mamlaka ya Iran na kwa nchi za Magharibi ambazo zina ushawishi kwa Israel, kuwataka wote kukomesha ongezeko hilo".