Sudan imekuwa vitani tangu April 15, 2023 baada ya jeshi la nchi hiyo na vikosi vya RSF kuanza mapigano nchini humo. / Picha: Reuters  

Pembezoni mwa nchi, katika eneo ambap.o mapigano yanaendelea, magari yanapita kwa kasi yakiwaancha wananchi, kwa hofu ya kusambaratishwa na vikosi vya wapiganaji ambavyo vinakaribia eneo hilo la kusini mwa nchi.

"Wameleta hali ya wasiwasi kabisa," amesema Rabab, ambae ni mkazi wa kijiji cha kaskazini cha Wad Madani, mji mkuu wa jimbo la Al-Jazirah na eneo ambalo limeshuhudia mapigano makali kati ya jeshi na vikosi vya RSF.

Kama alivyozungumza na AFP, alitaka kutambuliwa kwa jina moja tu kwa kuhofia kushambuliwa na wapiganaji ambao wamekuwa wakuwashambulia raia kwa zaidi ya miezi nane ya vita.

Siku ya Jumamosi, angala watu nane waliuawa na wapiganaji wa RSF katika kijiji cha Al-Jazirah, shuhuda ameiambia AFP, kuongeza kumesema walipigwa risasi walipojaribu kuwazuia kuiba.

300,000 wamekimbia makazi

Kusini mwa Khartoum, zaidi ya nusu milioni wametafuta makazi katika eneo la Al-Jazirah baada ya mapigano kupamba moto katika mji mkuu wa Sudan.

Mwezi huu, hata hivyo, vikosi vya wapiganaji viliingia ndani zaidi ya jimbo na kusambaratisha moja ya kambi chache zilizobaki nchini humo, na kusababisha watu 300,000 kukimbia tena, hayo ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Wale waliobaki-kwa kutaka au kutotaka kuondoka-wamejikuta katika kile Shirika la Msalaba Mwekundu unachosema "mtego wa kifo."

Tangu April 15, Sudan imeingia katika mapigano kati ya vikosi vya Abdel Fattah al-Burhan dhidi ya vile RSF vya aliyekuwa msaidi wake, Mohamed Hamdan Dagalo.

TRT Afrika